Tanzania na ukuaji wa soko la michezo ya kubashiri

Michezo ya kubashiri mitandaoni ni tasnia mpya nchini, kama ilivyo kwa nchi nyingi za Kiafrika. Licha ya upya wake, hii ni miongoni mwa tasnia inayokua kwa kasi zaidi hapa Tanzania.
Michezo ya kubahatisha mtandaoni inahusisha kubashiri matokeo ya michezo, kucheza kasino, michezo ya poka, roulette au michezo ya video za mitandaoni na michezo mingine. Lakini wateja wengi nchini hujihusisha zaidi na ubashiri wa matokeo ya michezo na kasino za mitandaoni.
Kushinda pesa kwenye bahati nasibu kunaweza kubadilisha maisha yako kwa namna nyingi. Zipo hadithi nyingi nzuri na zenye kuhamasisha kuhusu washindi wa michezo ya kubashiri mtandaoni ambao wametumia pesa zao vizuri na kubadilisha maisha yao na ya wale wanaowazunguka.
Mojawapo ya sababu zinazochangia zaidi kuongezeka kwa michezo ya kubashiri mitandaoni ni ukuaji wa utandawazi na teknolojia nchini uliotokana na uwepo wa kampuni bora na bunifu za michezo hiyo kama SportPesa.
Mwishoni mwa miaka ya 1990, Tanzania, kama nchi nyingine za Kiafrika iliruhusu bahati nasibu kwenye michezo na matumizi ya juu ya utumiaji wa mitandao nchini yaliambatana na kuhama kwa upepo wa namna ya kucheza michezo ya kubashiri kutoka madukani mpaka kwenye mtandao.
Mapinduzi haya yemetokana na uwekezaji mkubwa uliofanyika katika teknolojia na mifumo bunifu ya michezo hiyo iliyoletwa na SportPesa.
Kutokana na uwepo wa kampuni bora kama SportPesa, badala ya kupanga foleni katika majumba ya kuchezeshea michezo ya bahati nasibu au kasino za madukani, siku hizi wabashiri wanaweza kucheza kwa urahisi tu kupitia sehemu nyingi kwa kutumia simu ama kompyuta mpakato.
Kubashiri mtandaoni na teknolojia ya miamala ya pesa kwa njia ya simu
Ukuaji wa huduma za kutuma na kupokea pesa kwa njia ya simu za mkononi umekua ni mojawapo ya fursa adhimu kwa wafanyabiashara kuuza bidhaa na huduma zao kwa urahisi zaidi. Mojawapo ya sekta zinazonufaika zaidi kwa kupitia teknolojia hii ni ubashiri wa mtandaoni.
Miamala ya pesa kwa njia ya simu imekuwa ni njia ya malipo katika kampuni nyingi za kubashiri mtandaoni kama ilivyoelezwa hapo awali, michezo ya kubahatisha imekuwa kwa kasi zaidi kutokana na ongezeko la matumizi ya simu za mkononi, ongezeko la matumizi ya mitandao pamoja na huduma za kifedha za simu.