Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vigogo Simba waitana, mastaa wawekewa Sh450 milioni

VIGOGO Pict


SIMBA imefanikiwa kutinga fainali ya Kombe la Muungano, huku mabosi wa klabu hiyo wakiitana haraka kujadili mechi mbili ngumu dhidi ya Yanga zitakazochezwa ndani ya wiki moja.


Mwanaspoti linafahamu kuwa, viongozi wa klabu hiyo walirejea jijini Dar es Salaam mapema jana asubuhi, tayari kwa mkutano wa mipango na uamuzi uliokuwa ufanyike kuanzia saa 11 jioni.


Taarifa kutoka ndani ya Simba zimeeleza kuwa, mkutano huo ulikuwa na lengo la kuchora ramani kamili ya namna Wekundu hao wa Msimbazi watakavyoingia kwenye mechi hizo mbili dhidi ya Yanga, huku zote wakihitaji ushindi.

“Tunakutana leo (jana jioni) kujadili namna tutakavyoingia kwenye hizo mechi mbili. Unajua hizi ni mechi ngumu, lazima tujue namna ya kwenda kuwakabili hawa wapinzani wetu.

HESA 04

“Ukweli ni kwamba kuna mtego mkubwa sana kwenye hizi mechi mbili, kwa hiyo ni lazima tuingie kwa akili kubwa. Tukifanya kosa lolote tunaweza kujiingiza kwenye shida kubwa,” amesema kiongozi mmoja wa Simba.

Kuhusu hesabu za kuwakwepa Yanga, taarifa hizo zilieleza kuwa hakuna mpango wa namna hiyo, kwani Simba pia walikuwa na lengo la kufika fainali ya Kombe la Muungano na kushinda taji.

Kiongozi huyo ameongeza kuwa, Simba inataka kushinda mechi zote mbili na hakuna kabisa mpango wa kuwakwepa Yanga kukutana nao kwenye fainali.

MAE 01

“Hayo ni maneno tu. Unajua kila kitu kuhusu kupangwa kwa timu, sisi viongozi hatutaki kuhusika na lolote. Hayo ni majukumu ya kocha na wachezaji wake, hatuhusiki hata kidogo.

“Simba hatujashinda kombe lolote muda mrefu na hatuwezi kusema tuwaachie Kombe la Muungano halafu tujikite na ligi. Nani anajua kwamba tukikosa ubingwa tutakuwa na maana gani katika maamuzi hayo? Hakukuwa na hizo taarifa ndani,” amesema.

Katika hatua nyingine, Simba wamejipanga msimu huu, kwani hawajaingia kinyonge wameweka dau kubwa kwa wachezaji wao endapo watafanikiwa kushinda mbele ya Yanga.

HESA 01

Kama inavyofahamika bingwa wa Kombe la Muungano anaondoka na Sh150 milioni, lakini mabosi wa Simba wameweka Sh300 milioni kama pongezi kwa mastaa wao wakiibuka washindi, hivyo kufanya jumla mezani kuna Sh450 milioni.

“Viongozi wa Simba wameshawaambia wachezaji kuwa kama watashinda mechi ya dabi Jumatano, mpaka wanafika Dar es Salaam watakuwa wameshapokea bonasi yao mapema tu.

“Viongozi wanafanya hivyo kwa sababu wanataka kuwapa hamasa wachezaji kuelekea dabi ya pili. Kwa hiyo kazi imebaki uwanjani tu,” amesema.

Timu hizo zitakutana Aprili 29 mwaka huu kwenye fainali ya Kombe la Muungano itakayopigwa Uwanja wa Amaan, Zanzibar, kisha zitakutana kwenye Ligi Kuu Bara Mei 3, 2026 kwenye Uwanja wa Meja Generali Isamuhyo, Dar.