Viongozi BDL wahaha kutafuta saini

Muktasari:
- Wachezaji walionekana kuwa na wakati mgumu ni wachezaji wa Miyasi, Marcus Tshi, Emanuel Mulumba na Dan Mwendela raia wa Congo.
Viongozi wa timu zinazoshiriki ligi ya Mkoa wa Dar es Salaam (BDL), walikuwa wakipigana vikumbo kusaka saini za wachezaji wapya katika , wakati wa mashindano ya Ramadhani Star Ligi.
Wachezaji walionekana kuwa na wakati mgumu ni wachezaji wa Miyasi, Marcus Tshi, Emanuel Mulumba na Dan Mwendela raia wa Congo.
Mwanasposti ililokuwepo uwanjani hapo. lilishuhudia viongozi hao wakiwashawishi wachezaji hao wajiunge na timu zao.
Mmoja wachezaji hao, Mulumba alikiri kufuatwa ingawa hajataja majina ya viongozi hao; “Ni kweli nimefuatwa kuombwa na viongozi wanne nijiunge na timu zao.”
Jordan Jordan wa Mchenga Star anayecheza namba 4 ‘Power Forward’ alisema hajapata ofa yoyote hadi sasa na itakayokuja na nzuri atajiunga nayo.
“Timu itakayonihitaji na ofa nzuri nitajiunga kuchezea nayo msimu huu,” alisema Jordan.
Kocha wa mchezo huo kutoka Temeke, John Petar alisema ligi ya msimu huu itakuwa ngumu na timu ambayo haina fedha za kujiendeshea itashindwa kusajili nyota wakali.