Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga: Hatuiogopi Simba fainali, tunataka Kombe la Muungano

NTINE Pict

Muktasari:

  • Siku moja baada ya mchezo huo wakaibuka mabosi wa Yanga wakiongozwa na afisa mtendaji mkuu wa timu hiyo Mzambia Andrea Mtine, amesema timu yao haichagui ikutane na nani hata kama Simba itaingia basi wako tayari hakuna shida.

KUNA msimamo umetolewa na mabosi wa Yanga kisha akafuata kocha wa timu hiyo na kila mmoja utawahusu Simba wakisema hawana shida kama kutakuwa na dabi mbili ndani ya siku 10.

Yanga ilifuzu hatua na Fainali ya Kombe la Muungano juzi kwa mara ya pili mfululizo baada ya kuing'oa Azam FC kwa ushindi wa mabao 2-1, kwenye mchezo wa nusu fainali ya kwanza iliyopigwa Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Siku moja baada ya mchezo huo wakaibuka mabosi wa Yanga wakiongozwa na afisa mtendaji mkuu wa timu hiyo Mzambia Andrea Mtine, amesema timu yao haichagui ikutane na nani hata kama Simba itaingia basi wako tayari hakuna shida.

Mtine ameongeza wana timu imara ambayo inaweza kukutana na timu yoyote na kupata mafanikio na kutinga kwao fainali ni uhakika wanalitaka kombe hilo.

"Tunaposema Yanga bingwa tunamaanisha hivi, tunaweza kucheza mechi kubwa na kupata ushindi, sasa tumeingia fainali hatuwezi kuchagua nani aje lakini kama atakuja yeyote sisi tupo tayari," amesema Mtine.

"Kitu muhimu hapa kwetu sisi Yanga ni tunautaka ubingwa wetu, hilo ndio la msingi, tunamshukuru Mungu kwa namna timu yetu ilivyocheza vizuri leo tukionyesha ubora mkubwa kama mabingwa watetezi."

Kauli hiyo ya Mtine inakuja wakati ambao Simba jana usiku nayo ilikuwa uwanjani kwenye mechi ya nusu fainali ya pili la mashindano ya Muungano dhidi ya Mlandege ya Zanzibar.

Mshindi wa mechi hiyo ataifuata Yanga fainali itakayopigwa Aprili 29, hapahapa Uwanja wa Amaan na bingwa atajibebea kombe sambamba na Sh150 milioni.

Wakati Mtine akiyasema hayo, kocha wa timu hiyo, Pedro Goncalves akakoleza wino, haitakuwa mbaya kama watakutana na Simba ambao watakwenda kukutana nao mara ya pili ndani ya siku 10.

Pedro amesema kikosi chake kipo tayari kucheza na timu yoyote kati ya mbili zilizosalia na kama Simba itakata tiketi hiyo basi mashabiki watakwenda kufurahia kuona mechi kubwa mbili za timu kubwa.

"Siwezi kusema namtaka nani lakini yeyote atakayeingia fainali huyo ndio mpinzani wetu, sisi tupo tayari kukutana na timu yoyote, kama Simba akiingia itakuwa sawa kwani mashabiki watafurahia kuona mechi kubwa mbili za timu pinzani ndani ya siku 10,"amesema Pedro.

"Yanga tunataka mafanikio ya kuchukua kombe na bahati nzuri kwetu tumeimarika sana, tutakuwa na faida ya kutoka kucheza dabi dhidi ya Azam, pia tutakwenda kucheza dabi kubwa zaidi kama Simba ikiingia fainali."


Ibenge alia na mastaa Azam FC

AZAM imemaliza ushiriki wake kwenye mashindano ya Muungano juzi usiku baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Yanga, lakini kocha wake Florent Ibenge amelia na mastaa wake namna walivyocheza.

Matokeo hayo yanaifanya Azam kuendelea kusubiri kucheza fainali ya Kombe la Muungano taji ambalo bado litaendelea kukosekana kwenye mafanikio ya matajiri hao wa Chamazi.

Akizungumza na Mwanaspoti Ibenge raia wa DR Congo amesema bado anashangaa ni kitu gani kiliwakumba wachezaji wake walivyocheza chini ya kiwango kwenye dakika 45 za kwanza za mchezo huo.

Ibenge amesema wachezaji wake walicheza kwa tempa ya chini mithili ya kwamba wako mazoezini huku Yanga ikionyesha kiwango cha juu kama timu inayocheza mchezo wa nusu fainali.

"Hadi sasa sijafahamu nini chanzo cha wachezaji wangu kucheza chini namna ile kipindi cha kwanza, ilikuwa kama hatuchezi nusu fainali, ni kama tulikuwa kwenye mazoezi au mechi ya kirafiki wakati wenzetu wanacheza nusu fainali," amesema Ibenge.

"Angalau kipindi cha pili tuliamka kidogo na kupata bao moja, lakini kipindi cha kwanza tulicheza vibaya sana, hatukuonyesha kama ni timu inayotaka kuamua mechi, tulifanya makosa mengi.

"Tulikuwa tunajua Yanga ni wazuri kwa mashambulizi ya kushtukiza na sisi tukafanya makosa yaleyale ya kuwaruhusu kufanya mashambulizi ya aina hiyo kwa kupoteza mipira maeneo hatari.

Hata hivyo, Ibenge ambaye timu yake inashika nafasi ya tatu kwenye ligi amewashusha presha mashabiki wa Azam FC akisema wamejifunza kutokana  na makosa ambayo waliyafanya kwenye mechi hiyo na wanakubali kuondolewa kwenye mashindano.

"Tumejifunza kuna wakati unapata fundisho kutokana na kile unachofanya, tunatakiwa kuchukua hili somo gumu na kwenda kulifanyia kazi ili wakati mwingine isijirudie."