Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga: Hatuwaogopi Mamelodi

MTENDAJI Mkuu wa Yanga, Andrew Mtine amesema hawaiogopi Mamelod Sundowns waliyopangwa nayo kwenye hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, huku akitaja mambo matatu.

Mtine ameyataja mambo hayo kuwa wakiyafanya vizuri yatawanyoonyesha njia ya kuibuka na ushindi kwenye matokeo ya jumla na kutinga nusu fainali.

"Lazima tujiamini kwamba tunaweza kusonga mbele na wachezaji pia wajitolee kwa asilimia mia kupambana kwa ajili ya timu. Pia mashabiki nao wawe nyuma yetu kutusapoti," amesema.

"Tunaiheshimu Mamelod kwa ukubwa wao na mafanikio waliyoyapata, lakini hatuwezi kusema tunaenda kucheza nao tukiwa wanyonge. Itakuwa ni mechi kubwa acha tuone nini kitatokea."

Ikiwa itavuka katika hatua hiyo Yanga itakutana na mshindi kati ya Asec Memosa na Esperance de Tunis. Msimu huu Mamelod imeanza vizuri kwenye michuano ya kimataifa ikifanikiwa kuchukua ubingwa African Football League mbele ya Al Ahly.