Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga yaifata Ihefu kibabe

KLABU ya Yanga leo Desemba 20 asubuhi inaanza safari ya kwenda Mbeya kwa ajili ya mchezo wao ujao dhidi ya Ihefu utakaopigwa Desemba 23 katika Uwanja wa Highland Estate, Mbarali.

Safari hiyo itakuwa ni kwa gari na leo watalala Iringa kisha kesho asubuhi wataendelea na safari ya kwenda Mbeya.

Huo unakuwa ni mchezo wa pili kwa Yanga wakiwa ugenini baada ya awali kucheza na Mwadui wakishinda 5-0.

Yanga wanaenda Mbeya wakiwa na morali ya juu baada ya michezo miwili nje ya Dar es Salaam kutoka na ushindi (Mwadui 5-0, Dodoma Jiji 3-1 licha ya wao kuwa nyumbani).

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema safari hiyo inaanza mapema asubuhi ya leo na kisha timu watapumzika Iringa.

"Timu inaondoka leo asubuhi kwaajili ya kufika mapema Mbeya kujiandaa na mchezo dhidi ya Ihefu, kesho asubuhi tutaanza safari ya kwenda Mbeya," amesema Bumbuli

Bumbuli amesema baada ya mchezo huo wana kibarua kigumu dhidi ya Singida UTD kwenye Mashindano ya Azam Cup, kwani wanatakiwa warejee Dar es Salaam kwaajili ya mchezo huo.

"Ratiba imebana hatuwezi tukatoka Mbeya kisha tukaja Dar kucheza FA, kisha tukarudi tena Mbeya kucheza mchezo wa Ligi."

"Lakini kuna vikao ambavyo tutakaa kama Sekretarieti kuangalia kama tutapata usafiri wa ndege."

Yanga baada ya mechi na Singida ambayo itachezwa katikati ya Desemba 25-27, baada ya mchezo huo watakuwa na mchezo dhidi ya Prison Desemba 31 utakaopigwa Rukwa, Sumbawanga.

Wakati Yanga wakienda wakiwa na morali, Ihefu nao katika mchezo wao wa jana dhidi ya KMC walishinda 1-0.