Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yao Kouassi atulizwa Yanga, kocha ahusika

YAO Pict

Muktasari:

  • Yao aliyekuwa nje ya uwanja kwa miezi mitatu kutokana na kuumia nyama za paja, alianza mazoezi na wenzake, lakini juzi kati alijitonesha na kumfanya aendelee kukosekana uwanjani, huku ikielezwa kwa mechi zilizosalia za kufungia msimu sio rahisi kuziwahi tena, hivyo ni hadi msimu ujao.

YANGA ipo safarini kuifuata Fountain Gate kwa mchezo wa Ligi Kuu Bara inayopigwa Jumatatu, huku taarifa mbaya kwa mashabiki ni kwamba huenda wasimuone tena uwanjani beki wa kulia, Yao Kouassi aliyejitonesha jeraha.

Yao aliyekuwa nje ya uwanja kwa miezi mitatu kutokana na kuumia nyama za paja, alianza mazoezi na wenzake, lakini juzi kati alijitonesha na kumfanya aendelee kukosekana uwanjani, huku ikielezwa kwa mechi zilizosalia za kufungia msimu sio rahisi kuziwahi tena, hivyo ni hadi msimu ujao.

Beki huyo raia wa Ivory Coast amekuwa akiandamwa na majeraha tangu kuanza kwa msimu huu na kumfanya atumike katika mechi saba kati ya 25 za Ligi Kuu ilizocheza timu hiyo inayoongoza msimamo, ambapo pengo lake limezibwa na Israel Mwenda aliyeingia dirisha dogo na wakati mwingine Kibwana Shomary.

Taarifa kutoka ndani ya Yanga zinasema Yao ni kama hatacheza tena msimu huu baada ya kujitonesha jeraha hilo lililokuwa limeanza kupona wakati akijifua na wenzake mazoezini.

“Alikuwa ameshapona kabisa na kuanza mazoezi mepesi na yale magumu ya mwisho, lakini ghafla akaanza kusikia maumivu tena katika mguu wake na hivyo kuangaliwa upya na madaktari,” chanzo kililiambia Mwanaspoti na kuongeza:

“Bado haijajulikana atakaa nje kwa muda gani tena, lakini kwa jinsi hali yake ilivyo huenda akamaliza msimu akiwa nje, jambo linalomuumiza sana mchezaji mwenyewe.”

Kocha wa Yanga, Miloud Hamdi alilithibitishia Mwanaspoti kwamba, Yao anaendelea kujiuguza huku akiwa hajawahi kabisa kumtumia tangu ajiunge na timu hiyo kutokea Singida Black Stars kuchukua nafasi ya Sead Ramovic aliyetimkia CR Belouizdad ya Algeria.

Hamdi alisema anaelewa hali anayoipitia beki wake, lakini anahitaji muda zaidi ili awe sawa kabla ya kurudi uwanjani, hivyo kumtuliza presha aliyokuwa nayo kwa sasa baada ya kujitonesha.

“Namna tunaendelea kumtuliza Yao, kwa sababu anatamani sana kucheza. Kama unavyojua amekaa sana nje, ila anahitaji muda tena kwani mguu wake unamsumbua bado haujakaa sawa,” alisema Hamdi.

Katika nafasi ya beki ya kulia anayocheza Yao kwa sasa inatumiwa na Mwenda na Kibwana, huku mashabiki waliomzoea beki huyo maarufu kama jeshi wakiendelea kummkosa uwanjani.

Kibwana hadi sasa ametumika katika mechi saba kati ya 25 akitumia dakika 533 akiwa na asisti moja, wakati Mwenda amecheza mechi nane akitumia dakika 675 na kufunga mabao mawili bila ya kuwa na asisti yoyote.