Zahera ampa Balinya jukumu zito kwa Pyramids

Muktasari:
Balinya anarejea katika kikosi cha kwanza na kwenda kucheza kama mshambuliaji wa pili huku Tshishimbi akishuka na kwenda kucheza eneo la kiungo.
Dar es Salaam. Kocha Mwinyi Zahera amemwazisha mshambuliaji Juma Balinya katika kikosi cha kwanza cha Yanga kitakachoivaa Pyramids katika mchezo wa marudiano ya kombe la Shirikisho Afrika utakaofanyika saa 3:00 usiku jijini Cairo, Misri.
Balinya tangu ametua Yanga ameshindwa kuwa namba ya kudumu katika kikosi cha Zahera na kuzua maswali kuhusu uwezo wake.
Mfungaji bora huyo bora wa Ligi Kuu Uganda msimu uliopita, Balinya ndiye aliyefunga bao pekee la Yanga wakichapa Township Rollers katika mchezo wa awali wa Ligi ya Mabingwa uliofanyika Botswana.
Balinya anarejea katika kikosi cha kwanza na kwenda kucheza safu ya ushambuliaji wa Yanga akiwa pamoja Sadney Urikhob huku Tshishimbi akishuka na kwenda kucheza eneo la kiungo.
Balinya na Sadney wakiwa mbele nyuma yao atakuwepo nahodha Papy Tshishimbi mfungaji wa bao pekee la Yanga katika mchezo uliopita uliofanyika jijini Mwanza.
Kocha Zahera amefanya mabadiliko ya wachezaji watatu walioanza katika mchezo uliopita, na kuingiza wapya.
Katika kikosi kinachoanza leo wachezaji Kelvin Yondani, Feisal Salum na Mrisho Ngassa wameondolewa katika kikosi cha kwanza.
Yondani aliyepata kadi nyekundu katika mchezo uliopita nafasi yake imechukuliwa na Lamine Moro, wakati Deus Kaseke akichukua nafasi ya Ngassa aliyesababisha bao la pili la Pyramids katika mchezo uliopita, huku Balinya akichukua nafasi ya Fei Toto.
Kikosi kinachoanza leo Faroukh Shikhalo, Juma Abdul, Ally Mtoni, Ally ally, Lamine Moro, Abdullaziz Makame, Deus Kaseke, Papy Tshishimbi, Sadney Urikhob, Juma Balinya na Mapinduzi Balama.
Kikosi kilichocheza mchezo nchini Tanzania, Faroukh Shikhalo, Juma Abdul, Ally Mtoni, Ally Ally, Kelvin Yondani, Feisal Salum, Mrisho Ngassa, Abdullaziz Makame, Sadney Urikhob, Papy Tshishimbi na Mapinduzi Balama.