Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Zitto: Prof Sarungi asingekubali Bodi ya Ligi kuahirisha Dabi ya Kariakoo

Muktasari:

  • Zitto amesema  Mzee Sarungi alikuwa ni shabiki mkubwa wa Simba na alijulikana kwa msimamo wa kutotaka kuona ligi ya Tanzania ikiporomoka au kupuuziliwa mbali na klabu mbili tu za Simba na Yanga.

KIONGOZI Mstaafu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amesema kama Profesa Mzee Philemon Sarungi angekuwa hai, angekemea kwa ukali uamuzi wa kuahirisha mechi ya dabi kati ya Yanga na Simba iliyokuwa ichezwe Jumamosi, Machi 8, kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa, Dar es Salaam, akisisitiza uamuzi huo haukufaa kwa masilahi ya Ligi ya Tanzania.

Zitto amesema  Mzee Sarungi alikuwa ni shabiki mkubwa wa Simba na alijulikana kwa msimamo wa kutotaka kuona ligi ya Tanzania ikiporomoka au kupuuziliwa mbali na klabu mbili tu za Simba na Yanga.

"Sina hakika kama Mzee Sarungi angekuwepo juzi tulipotangaziwa kwamba mechi ya Dabi ya Simba na Yanga imeahirishwa angereact (angechukua hatua) namna gani, kwa sababu mzee alikuwa ni mnazi wa Simba kwelikweli, lakini naamini asingekubali upuuzi wowote ule wa kuifanya ligi yetu ionekane haina maana na inaendeshwa na klabu mbili tu kati ya 16 zinazoshiriki ligi hiyo," amesema Zitto.

Zitto ameyasema hayo leo, Jumatatu, Machi 10, 2025, kwenye viwanja vya Karimjee, Dar es Salaam, wakati wa kuaga mwili wa Profesa Sarungi aliyefariki dunia Machi 5, mwaka huu jijini Dar es Salaam.