Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ndayiragije akuna mabosi, kulamba dili jipya

Ndayiragije Pict

Muktasari:

  • Kocha huyo raia wa Burundi aliyewahi kuzinoa Mbao FC, Azam FC na KMC zilizopo Ligi Kuu Bara amekuwa kocha wa nane wa Police FC katika miaka mitatu akichukua nafasi ya Salim Babu aliyetimuliwa kufuatia matokeo mabaya na Mrundi huyo alipewa mkataba wa miezi sita.

MABOSI wa Police FC ya Kenya wanatarajiwa kumsainisha mkataba mpya wa mwaka mmoja kocha mkuu Etienne Ndayiragije baada ya kuridhishwa na utendaji wake wa kazi tangu alipotua katika kikosi hicho kinachoshiriki Ligi Kuu Kenya (FKF-PL).

Kocha huyo raia wa Burundi aliyewahi kuzinoa Mbao FC, Azam FC na KMC zilizopo Ligi Kuu Bara amekuwa kocha wa nane wa Police FC katika miaka mitatu akichukua nafasi ya Salim Babu aliyetimuliwa kufuatia matokeo mabaya na Mrundi huyo alipewa mkataba wa miezi sita.

Mwenyekiti wa klabu hiyo, Munga Nyale amethibitisha matarajio ya kumsainisha Ndayiragije mkataba mpya alipokuwa katika hafla ya chakula cha jioni na klabu hiyo iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena, Nairobi.

"Mkataba wa miezi sita wa kocha utaongezwa. Lengo letu ni kumaliza mwaka huu tukiwa vinara wa ligi na tuendelee kuwa hivyo kwa miaka mitano ijayo ili kufanya Police FC kuwa timu inayoheshimika," amesema Nyale.

Pia amezungumzia malengo ya klabu kufuzu michuano ya kimataifa na kuongeza idadi ya mashabiki wake, huku akifichua kuwa Police TV itazinduliwa hivi karibuni.

Wakati Ndayiragije alipochukua timu Novemba, mwaka jana, Police FC ilikuwa ikishika nafasi ya 15 kwa kuwa na pointi nane baada ya kuchezo michezo saba, ikipata ushindi mmoja, sare nne na kufungwa mechi mbili.

Kwa sasa timu imepanda hadi kileleni mwa msimamo wa FKF-PL ikiwa na pointi 38 baada ya mechi 20 sawa na Tusker FC, lakini inaongoza kwa tofauti ya mabao (+5).

Chini ya Ndayiragije aliyewahi pia kuinoa timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' na kuipeleka Fainali za Chan 2020, Police FC imeshinda mechi 10, sare nane na kupoteza mechi mbili.