Alvarez sasa aingia anga za mabosi wa FC Barcelona

Muktasari:

  • Hivi karibuni Alvarez alikuwa akitajwa huenda angetua Atletico lakini yeye mwenyewe alisema kwamba hafikirii kuondoka kwa sasa.

BAADA ya Atletico Madrid sasa Barcelona imejitosa katika mchakato wa kutaka kumsajili straika wa Manchester City na  Argentina, Julian Alvarez, 24, katika dirisha hili na inaweza kumtumia Lionel Messi kumshawishi staa huyo ambaye kwa sasa yupo naye katika kambi ya timu ya taifa akubali ofa ya kujiunga na wababe hao wa Catalunya.

Hivi karibuni Alvarez alikuwa akitajwa huenda angetua Atletico lakini yeye mwenyewe alisema kwamba hafikirii kuondoka kwa sasa.

Moja ya sababu zilizotajwa kwamba zinaweza kumshawishi staa huyu kutaka kuondoka ni kupata timu itakayompa nafasi ya kutosha tofauti na ilivyo sasa ambapo amekuwa akitumika zaidi pale Erling Haaland anapokosekana.

Hata hivyo, haionekani kama Barcelona inaweza kutoa kiasi cha pesa kitachohitajika na Man City ili kumuuza kutokana na hali yao ya kiuchumi kwa sasa.

Ingawa haijawekwa wazi lakini tovuti nyingi zinadai Barcelona inataka kumchukua kwa mkopo staa huyu ambaye mkataba wake unamalizika mwaka 2028.

Mwamba huyo ameshinda takriban mataji yote ya soka aliyowania.