Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Amorim adai Man United ni bora isifuzu Uefa

Muktasari:

  • Hata hivyo, kocha Amorim alisema kubeba taji hilo kuna maana ya kushinda tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao – lakini si matokeo anayohitaji kwa sasa katika kipindi cha kukijenga kikosi.

MANCHESTER, ENGLAND: KOCHA, Ruben Amorim anafahamu wazi presha atakayokabiliana nayo endapo kama Manchester United haitanyakua taji la Europa League, Jumatano ijayo.

Hata hivyo, kocha Amorim alisema kubeba taji hilo kuna maana ya kushinda tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao – lakini si matokeo anayohitaji kwa sasa katika kipindi cha kukijenga kikosi.

Kocha huyo Mreno anafahamu wazi anahitaji muda wa kutosha wa kufanya kazi ya kukifuma upya kikosi hicho kuliko kujiongezea mzigo wa mechi nyingine nane za Ligi ya Mabingwa Ulaya kwenye hatua ya ligi msimu ujao, kutatibua mipango yake.

Lakini, tatizo Man United ipo kwenye nafasi ya 16 katika msimamo wa Ligi Kuu England, ikiwa ni habari mbaya kabisa kwenye historia yao katika zama hizi. Kutokana na hilo, Amorim anafahamu wazi hana chaguo jingine zaidi ya kupata ushindi tu huko Bilbao kutakakofanyika fainali ya Europa League dhidi ya Tottenham Hotspur wiki ijayo.

Alipoulizwa kuhusu presha itakayomkabili endapo Man United itashindwa kuifunga Spurs, Jumatano ijayo, alisema: “Ndiyo, ni kubwa kama hatutashinda. Lakini, siwazii juu ya hilo. Itakuwa mbaya kama Man United itapoteza. Sitaki hii ionekane kama kisingizio, lakini hali itakwenda kuwa ngumu sana. Hizo ni hisia zangu. Uvumilivu wa mashabiki na nyie watu, ina maana msimu ujao tutapaswa kuwa makini sana.”

Kocha Amorim anafichua kwamba anadhani ingekuwa vyema kama Man United isingekuwa na majukumu ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao, aliposema: “Hayo ni maoni yangu - tunahitaji muda zaidi kwenye hii timu. Tunahitaji kuweka mambo mengi sawa mazoezini Carrington na isiwe mechi baada ya mechi. Pia kuna kikosi. Tumeonyesha msimu huu, inahitaji kuwa na kikosi bora kushinda mechi za Ulaya.”