Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Amorim anamtaka fundi Trincao aje

AMORIM Pict
AMORIM Pict

Muktasari:

  • Kocha huyo Mreno anahitaji mchezaji wa pembeni baada ya Jadon Sancho na Marcus Rashford kuonekana kutokuwa na uhakika wa kurudi tena Old Trafford baada ya dili zao za mikopo kumalizika mwishoni mwa msimu huu.

MANCHESTER, ENGLAND: KOCHA wa Manchester United, Ruben Amorim amepanga kufanya usajili wa winga wa Sporting Lisbon, Trincao kwenye dirisha lijalo la majira ya kiangazi huku Mreno huyo akidaiwa kuuzwa Pauni 35 milioni.

Kocha huyo Mreno anahitaji mchezaji wa pembeni baada ya Jadon Sancho na Marcus Rashford kuonekana kutokuwa na uhakika wa kurudi tena Old Trafford baada ya dili zao za mikopo kumalizika mwishoni mwa msimu huu.

Trincao, ambaye alifunga mabao mawili wakati Ureno ilipoichapa Denmark mabao 5-2 kwenye Nations League Jumapili iliyopita, hilo limewafanya mabosi wa Man United kumweka mchezaji huyo kwenye orodha ya inaowasaka.

Trincao, 25, aliwahi kuwa na kipengele kinachohitaji ilipwa Pauni 400 milioni kuvunja mkataba wake wakati alipohamia Barcelona, lakini maisha yake huko hayakuwa mazuri na kuishia kwenda kwa mkopo Wolves.

Baada ya msimu mmoja Sporting, Amorim aliamua kumchukua mchezaji huyo jumla wakati alipokuwa akiinoa miamba hiyo ya Ureno kabla ya kunasa kibarua cha Old Trafford.

Trincao ni winga wa kulia anayetumia mguu wa kushoto, lakini anaweza kucheza pande zote za pembeni na amekuwa akitumika pia kwenye kucheza kati. Newcastle na Arsenal nazo zimekuwa zikimhitaji mchezaji huyo.

Hata hivyo, tishio kubwa linaweza kuwa Barca, ambao wameweka kipengele cha kumnunua wao kwanza kama Sporting itataka kumuuza tena kwa ada isiyozidi Pauni 20 milioni.

Lakini, kocha Amorim anaamini kwenye uhusiano wake mzuri wa kufanya kazi na mchezaji huyo unaweza kumfanya Trincao akubali kutua Old Trafford.