Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ancelotti hatarini kufungwa jela

Muktasari:

  • Kocha huyo wa Real Madrid, Ancelotti kesi yake itasikilizwa Jumatano ijayo.

MADRID, HISPANIA: KOCHA Carlo Ancelotti amejiweka kwenye hatari ya kufungwa jela kwa zaidi ya miaka minne baada ya kudaiwa kukwepa kulipa kodi, mahakama moja ya Hispania imefichua.

Kocha huyo wa Real Madrid, Ancelotti kesi yake itasikilizwa Jumatano ijayo.

Ancelotti kwa sasa yupo kwenye kikosi cha Los Blancos ikiwa ni awamu yake ya pili baada ya kurudi kwenye timu hiyo mwaka 2021. Hata hivyo, tuhuma hizo zinazomkabili Ancelotti ameripotiwa kuzifanya kwenye awamu yake ya kwanza aliyokuwa kwenye kikosi hicho cha Bernabeu.

Kwa mujibu wa AFP, ilibainisha taarifa ya mahakama ya Hispania, Ancelotti anashutumiwa kushindwa kubainisha malipo yake halisi aliyokuwa akivuna kupitia haki yake ya taswira mwaka 2014 na 2015. Amedaiwa jambo hilo limeikosesha mamlaka ya kodi ya Hispania zaidi ya Euro 1 milioni.

Kocha Ancelotti aliulizwa juu ya jambo hilo mwaka 2024, wakati kikosi cha Real Madrid kilipokwenda kushinda ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, alisema: "Hizo ni stori za zamani, hazinisumbui, naamini zitamalizwa haraka."

Aliongeza: "Nimeamua kuwa mtulivu na tatizo ni kwamba vitu vinaibuka wakati timu inapofanya vizuri."

Ancelotti alishinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya kwenye awamu yake ya kwanza Real Madrid, shukrani kwa ushindi katika mechi ya dakika 120 dhidi ya Atletico Madrid. Ameongeza ushindi mara mbili wa taji hilo baada ya kurudi Bernabeu, alipoichapa Liverpool kwenye fainali 2022 na Borussia Dortmund mwaka jana, 2024.

Msimu huu, Real Madrid bado ipo kwenye mchakamchaka wa kufukuzia ubingwa wa taji hilo la Ligi ya Mabingwa Ulaya na kwenye hatua ya robo fainali itakipiga na Arsenal baada ya kuzisukuma nje vigogo Manchester City na Atletico.

Kwenye La Liga, kikosi cha Real Madrid kilitarajiwa kukipiga na Leganes, Jumamosi kikijaribu kukimbizana na Barcelona kwenye mbio za ubingwa wa ligi hiyo.