Diallo ashusha presha Man United

Muktasari:
- Mchezaji huyo wa pembeni mwenye umri wa miaka 22 amekuwa nje ya uwanja tangu mapema Februari mwaka huu kutokana na majeraha ya kifundo cha mguu wakati wa mazoezi kabla ya mechi ya Ligi Kuu dhidi ya Tottenham.
MANCHESTER, ENGLAND: MANCHESTEER United imepata nguvu ya kutosha ikielekea kumaliza msimu baada ya kutoka kwa taarifa njema kuhusu majeraha ya staa wake, Amad Diallo.
Mchezaji huyo wa pembeni mwenye umri wa miaka 22 amekuwa nje ya uwanja tangu mapema Februari mwaka huu kutokana na majeraha ya kifundo cha mguu wakati wa mazoezi kabla ya mechi ya Ligi Kuu dhidi ya Tottenham.
Awali, ilisemwa kwamba huenda asionekane tena akicheza msimu huu jambo ambalo lilikuwa pigo kubwa kwa Man United kwani staa huyu alikuwa mchezaji tegemeo akifunga mabao tisa na kutoa asisti saba katika mashindano yote.
Hata hivyo, Amad ameonekana kupona haraka kwa juhudi zake mwenyewe na madaktari wa timu.
Urejeo wa fundi huyu unaonekana kuwa utaisaidia sana Man United katika michuano ya Europa League ambako imehamishia nguvu baada ya kufanya vibaya katika ligi hadi sasa.
Kwa mujibu wa mwandishi, Fabrizio Romano, Amad anatarajiwa kurejea uwanjani wiki ijayo licha ya ripoti za awali zilizodai kwamba msimu wake ulikuwa umekwisha kutokana na majeraha.
"Amepona kwa haraka… na hivyo atakuwa na uwezo wa kujiunga na mazoezi kuanzia wiki ijayo."
Man United itasafiri hadi Bournemouth Jumapili, kisha itakutana na Athletic Bilbao katika nusu fainali ya Europa League Mei mosi.