Anabaki! Mo Salah miwili tena

Muktasari:
- Nyota huyo wa kimataifa wa Misri mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwisho wa msimu huu na dili hilo jipya litamfanya aendelee kukipiga Anfield hadi mwaka 2027.
LIVERPOOL, ENGLAND: ANABAKI. Ndicho unaweza kusema baada ya tetesi nyingi kumhusisha Mohamed Salah na matajiri wa Saudi Arabia, lakini kilichoko ni anakaribia kusaini dili la mkataba mpya wa miaka miwili utakaomfanya alipwe zaidi ya Pauni 42 milioni.
Nyota huyo wa kimataifa wa Misri mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwisho wa msimu huu na dili hilo jipya litamfanya aendelee kukipiga Anfield hadi mwaka 2027.
Mkurugenzi wa michezo wa Liverpool, Richard Hughes ameanzisha mazungumzo na wakala wa Salah, Ramy Abbas Issa na mambo yamefikia patamu.
Salah aliwahi kudai uwezekano wa kuondoka Liverpool ni mkubwa kuliko kubaki na alikuwa amewekewa pesa nyingi na klabu za Saudia, kabla ya sasa kuibuka kwa taarifa hizi za kubaki na anatarajiwa kusaini mkataba utakaomfanya alipwe takriban Pauni 400,000 kwa wiki.
Taarifa hizo ni kama tulizo kwa mashabiki wa klabu hiyo ambao wametoka pia kusikia kuhusu nyota wao mwingine, Virgil van Dijk ambaye mkataba wake unaisha mwisho wa msimu akidai wawakilishi wake wameshaanza mazungumzo ya mkataba mpya na Liverpool na anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka miwili.
Kulikuwa na hofu nyota hao pamoja na Trent Alexander-Arnold ambaye anapewa nafasi kubwa ya kwenda Real Madrid, wote wangeondoka kama wachezaji huru msimu lakini mambo yanaonekana kubadilika.
Timu za Saudia zilitaka kumsajili Salah tangu mwaka 2023 na Al Ittihad iliweka mezani ofa inayokaribia Pauni 150 milioni ili kuipata huduma yake lakini ilikataliwa na Liverpool.
Pigo pekee ambalo majogoo hawa wanaonekan kuwa watalipata ni kuondoka kwa beki wao aliyekuzwa katika akademi yao Trent Alexander-Arnold ambaye ameonyesha dalili zote za kutaka kuondoka huku Real Madrid ikitajwa kuwa itamsajili.
Ingawa hajasaini mkataba na Madrid, lakini inasemekana vigogo hao wa Hispania wana ‘uhakika’ mchezaji huyo wa miaka 26 ataungana nao mara baada ya mkataba wake wa Liverpool kumalizika.
Ikiwa hilo litafanikiwa, Alexander-Arnold atakuwa mchezaji wa saba raia wa England kucheza Real Madrid, sawa na mastaa wengine waliowahi kufanya hivyo wakiwamo wawili wa klabu hiyo, Steve McManaman na Michael Owen.
Hata hivyo, Liverpool bado inaweza kupata pesa katika dili hilo la Madrid baada ya dirisha la uhamisho jipya kutangazwa kwa timu kusaini na kuuza wachezaji kabla ya Kombe la Dunia la Klabu, ambalo Real inashiriki.
“uhakika” mchezaji huyo wa miaka 26 ataungana nao mara baada ya mkataba wake wa Liverpool kumalizika.
Ikiwa hilo litafanikiwa, Alexander-Arnold atakuwa mchezaji wa saba raia wa England kucheza Real Madrid, akiungana na mastaa wengine waliowahi kufanya hivyo kama Steve McManaman na Michael Owen ambao walitokea Liverpool.
Hata hivyo, Liverpool bado inaweza kupata ada kwenye dili hili baada ya dirisha la uhamisho jipya kutangazwa kwa timu kusaini na kuuza wachezaji kabla ya Kombe la Dunia la Klabu, ambalo Real wanashiriki.