Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arsenal yapoteza mtu nyuma ya Mikel Arteta

ARSENAL Pict

Muktasari:

  • Allen alijiunga na klabu hiyo 2017 na baadaye alipandishwa kuwa mkuu wa idara 2022, akifanya kazi kwa karibu na kocha Mikel Arteta kwa takribani miaka sita na nusu. Kuondoka kwake kunafuatia pia kiongozi mwingine wa benchi la ufundi, daktari mkuu, Zafar Iqbal, aliyeondoka hivi karibuni.

LONDON, ENGLAND: KUNA mabadiliko mengine ya kiutendaji nyuma ya pazia katika timu ya Arsenal, huku msimu wa majira ya kiangazi wa kuondoka kwa baadhi ya wafanyakazi ukiendelea.

Mkuu wa sayansi ya michezo na utendaji, Tom Allen, anatarajiwa kuondoka klabuni hapo baada ya takribani muongo mmoja akiwa na Gunners.

Allen alijiunga na klabu hiyo 2017 na baadaye alipandishwa kuwa mkuu wa idara 2022, akifanya kazi kwa karibu na kocha Mikel Arteta kwa takribani miaka sita na nusu. Kuondoka kwake kunafuatia pia kiongozi mwingine wa benchi la ufundi, daktari mkuu, Zafar Iqbal, aliyeondoka hivi karibuni.

Arsenal, ambao walimaliza ukame wa miaka 22 bila ubingwa wa Ligi Kuu England msimu uliopita, walikumbwa na majeraha mengi kwa wachezaji muhimu kama Bukayo Saka na nahodha Martin Odegaard. Inaaminika klabu hiyo inafanya mabadiliko ili kuepuka changamoto hizo msimu ujao.

Kwa upande wa uwanja, Arsenal tayari wameanza usajili wa majira ya kiangazi kwa kufanya uhamisho wa mkopo wa Piero Hincapie kutoka Bayer Leverkusen kuwa wa kudumu kwa dau la Pauni 34.5 milioni, ambapo beki huyo wa kushoto kutoka Ecuador alicheza mechi 39 katika mashindano yote msimu wa 2025/26 na kuwa miongoni mwa nguzo muhimu katika mafanikio ya Arsenal.

ARS 01

Arsenal pia wanahusishwa na wachezaji kadhaa wakubwa akiwemo kiungo wa Newcastle United na Brazil, Bruno Guimarães, pamoja na kiungo wa Bournemouth Alex Scott. Mshambuliaji wa PSG na Ufaransa, Bradley Barcola naye anatajwa kuwa miongoni mwa walengwa, huku pia Morgan Rogers wa Aston Villa akiwa kwenye orodha ya wachezaji wanaotakiwa.

Arteta amekaririwa akisema baada ya kushindwa kwao katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kuwa timu ni lazima ichukue uamuzi mgumu ili kupiga hatua zaidi. Arsenal itaanza kutetea ubingwa wa Ligi Kuu England msimu wa 2026/27 kwa mchezo wa ufunguzi dhidi ya Coventry City Agosti 21. Kabla ya hapo, itacheza na Manchester City katika Ngao ya Jamii kwenye Uwanja wa Wembley.

Mkataba wa Arteta unamalizika mwisho wa msimu ujao, lakini uongozi wa klabu una imani anaweza kuongeza muda wa kubaki Emirates.