Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arteta adai Havertz, Gabriel kutibua usajili

Muktasari:

  • Kocha Arteta bado anakuna kichwa baada ya beki wake Mbrazili, Gabriel kukosekana uwanjani na kwamba atafanyiwa upasuaji wa misuli ya paja kutibu majeraha aliyopata kwenye mechi ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Fulham, Jumanne iliyopita.

LONDON, ENGLAND: KOCHA wa Arsenal, Mikel Arteta amesema kuna swali zito juu ya hali za wachezaji Kai Havertz na Gabriel baada ya kufanyiwa upasuaji na kwamba wakali hao wanaweza kuwa na athari kubwa kwenye mipango yao ya usajili ujao.

Kocha Arteta bado anakuna kichwa baada ya beki wake Mbrazili, Gabriel kukosekana uwanjani na kwamba atafanyiwa upasuaji wa misuli ya paja kutibu majeraha aliyopata kwenye mechi ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Fulham, Jumanne iliyopita.

Beki huyo sasa anakwenda kuungana na straika Havertz kwenye chumba cha wagonjwa baada ya Mjerumani huyo naye kufanyiwa upasuaji wa misuli, Februari mwaka huu, huku mshambuliaji Gabriel Jesus na beki Takehiro Tomiyasu nao wakiwa nje ya uwanja hadi mwisho wa mwaka 2025.

Kocha Arteta hivi karibuni aliwahi kusema dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi linakwenda kuwa kubwa sana, wakati miamba hiyo ya Emirates ikimkaribisha klabuni bosi mpya wa usajili, mkurugenzi wa michezo, Andrea Berta — ambaye atakuwa na kazi kubwa ya kusajili Namba 9 wa viwango.

Lakini, Arteta sasa anafunguka kwamba ishu ya usajili itategemea na Gabriel na Havertz watarudi wakati gani uwanjani kama katika kipindi cha pre-season au kama watahitaji kufanya usajili wa wachezaji wengi zaidi.

Wakati Arsenal ikijiandaa na mechi dhidi ya Everton kwenye Ligi Kuu England iliyofanyika Jumamosi, kocha Arteta alisema ishu ya usajili kwenye dirisha lijalo itategemea na hali ya wachezaji majeruhi waliopo kwenye kikosi chao.

Alisema: "Itakwenda kuwa ngumu sana. Kuna wachezaji wataanza msimu wakitokoea kufanyiwa upasuaji, hivyo hilo linatuacha kwenye maswali magumu sana. Hatujui kama wataweza kurudi na kuwa na kitu kwenye timu. Ngoja tuone, hilo litaathiri kiasi gani mpango wetu wa usajili."

Arsenal sasa ina wachezaji wanne ambao wamekumbana na matatizo ya misuli ya paja msimu huu. Gabriel Martinelli alikuwa nje ya uwanja kwa mwezi mzima mwaka huu, wakati Bukayo Saka alirejea uwanjani wiki iliyopita baada ya kuwa nje ya uwanja tangu Desemba mwaka jana.