Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arteta avaa gwanda kwa Nico Williams

ARTETA Pict

Muktasari:

  • Arsenal wanatarajia kumrudisha Bukayo Saka kutoka kwenye majeraha makubwa ya misuli ya paja kabla ya mechi yao ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Real Madrid mwezi ujao.

LONDON, ENGLAND: KOCHA wa Arsenal Mikel Arteta anadaiwa kuwasiliana na wawakilishi wa winga wa  Athletic Bilbao, Nico Williams, ikiwa ni katika mipango yake ya kutaka kumsajili katika dirisha la majira ya kiangazi mwaka huu.

Arteta amechukua jukumu la kuvaa magwanda mwenyewe na kujaribu kupiga simu kwa wawakilishi wa Nico na Nico mwenyewe baada ya kupitia changamoto nyingi msimu huu ambapo mastaa wengi wamekuwa wakisumbuliwa na majeraha hali iliyosababisha wapate changamoto katika mbio zao za ubingwa.

Kwa mujibu wa tovuti ya Bild, katika mkataba wake  winga huyo ana kipengele kinachomruhusu kuondoka ikiwa timu inayohitaji huduma yake italipa kati ya Oauni 48 milioni hadi Pauni 67 milioni.

Hata hivyo, Arsenal siyo klabu pekee inayotaka kumsajili Williams, kwani Bayern Munich pia inasemekana kuwa na nia ya kumsajili ikiwa pamoja na Barcelona, Liverpool, na Chelsea.

Williams angeweza kuondoka Bilbao msimu uliopita baada ya kung'ara sana akiwa na timu ya taifa ya Hispania katika mashindano ya  Euro 2024, lakini alichagua kubaki kwenye timu hiyo.

Alipoulizwa kuhusu uwezekano wa kuondoka katika kikosi cha Athletic Nico Agosti mwaka jana alisema:"Ni vizuri kuona timu kubwa zinahusishwa nawewe, lakini nimekuwa wazi kila wakati kwamba nataka kuendelea kuwa hapa,"

"Athletic Club ni sehemu tofauti ambayo siwezi kuipata katika klabu zingine. Najiandaa kufanya mambo makubwa katika klabu hii.  Kulikuwa na maombi kutoka kwa klabu nyingi. Moyo wangu uko na Athletic. Nina mkataba hapa, lakini nani ajuaye kinachoweza kutokea baadaye. Nilikuwa na hamu ya kubaki kwa sababu kucheza Ulaya na Athletic Club ndiyo kitu kilichonifurahisha zaidi." 

Arsenal wanatarajia kumrudisha Bukayo Saka kutoka kwenye majeraha makubwa ya misuli ya paja kabla ya mechi yao ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Real Madrid mwezi ujao.

"Atakuwa hapa kwenye uwanja wa mazoezi wa Arsenal wiki ijayo, na tunatarajia atakuwa na uwezo wa kuuchezea mpira kuliko ilivyokuwa," Arteta alisema alipoulizwa kuhusu hali ya majeraha ya Saka.