GABOR: Mwamba wa Hungary na rekodi ya miaka minane Euro

Muktasari:

  • La kuvutia zaidi kwenye fainali hizi ni rekodi mbalimbali zinazowekwa, tukishuhudia ile ya mchezaji mwenye umri mdogo zaidi kufunga bao kwenye mchezo wa kwanza wa ufunguzi wa michuano hiyo iliyokuwa ikishikiliwa na Cristiano Ronaldo ya miaka 19 na siku 128 na kuvunjwa na kinda wa Arda Guller aliyefanya hivyo akiwa na umri wa miaka 19 na siku 114.

FAINALI za Kombe la Mataifa ya Ulaya (Euro 2024) zinaendelea Ujerumani na mambo mengi yametokea ikiwa hatua ya makundi imekamilika kwa mechi za jana, Jumatano.

La kuvutia zaidi kwenye fainali hizi ni rekodi mbalimbali zinazowekwa, tukishuhudia ile ya mchezaji mwenye umri mdogo zaidi kufunga bao kwenye mchezo wa kwanza wa ufunguzi wa michuano hiyo iliyokuwa ikishikiliwa na Cristiano Ronaldo ya miaka 19 na siku 128 na kuvunjwa na kinda wa Arda Guller aliyefanya hivyo akiwa na umri wa miaka 19 na siku 114.

Michuano hiyo iliyoanza mwaka 1955 inazidi kutengeneza rekodi miongoni ikiwa ni ile ya kuwa na mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi katika historia ya fainali hizo, Kepler Ferreira ‘Pepe’ wa kikosi cha Ureno.

Pepe aliingia uwanjani akiwa na umri wa miaka 41 na siku 113 akiivunja rekodi ya kipa Gabor Kiraly wa Hungary aliyecheza mashindano ya Euro 2016, Ufaransa akiwa na umri wa miaka 40 na siku 86.

Leo nitamzungumzia huyu mchezaji wa Hungary ambaye alikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kumpongeza Pepe.

“Umeivunja rekodi yangu. Hongera na sisikitiki kwa vile na mimi niliivunja rekodi iliyodumu kwa miaka 16 iliyokuwa imewekwa na kiungo wa Ujerumani, Lothar Matthaus. Lakini ujue na hii yako itavunjwa, ingawa sio kazi rahisi,” alimwambia.

Kipa huyu wa Hungary alifanya makubwa, lakini hakuwa anavuma sana isipokuwa kuzungumzwa sana kwa kivazi chake cha suruali nyepesi ya rangi ya kijivujivu iliyofanana na vazi la kulalali (pajama).

Kiraly alizichezea klabu mbalimbali na timu ya taifa ya Hungary kwa kipindi cha miaka 25, zikiwamo Crystal Palace, West Ham United, Aston Villa, Burnley na Fulham za England akicheza mechi 830 na kati ya hizo, 104 akiwa na Palace.

Kabla ya hapo alizichezea klabu mbalimbali za Ujerumani zinazoshiriki Ligi Kuu ya Bundesliga kuanzia mwaka 2004 hadi 2009.

Alianza kuichezea timu ya taifa ya Hungary Machi 25, 1998 dhidi ya Austria katika heka heka za kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia na kuibuka na ushindi wa 3-2, akiweka kumbukumbu ya kuzuia mkwaju wa penalti dakika nne tu baada ya mchezo kuanza.

Mara nyingi akiwa uwanjani, mashabiki walitamani kumwona akiwa ameacha kuvaa suruali yake ya kijivujivu inayofanana na pajama aliyoivaa kwa takribani miaka 20 na kabla ya kuwa nayo alikuwa akivaa rangi tafauti karibu kila mchezo.

Hata hivyo, aliamua kuchagua rangi nyeusi na aliiona nuksi kwani mara sita akiwa golini na suruali hiyo nyeusi alifungwa mabao ya kipuuzi.

Tangu alipostaafu rasmi soka Kiraly amekuwa akisimamia klabu yake ya mpira iitwayo Király SZE aliyoianzisha mwezi Mei, 2019 kwao alikozaliwa, mji mdogo wa Szombathely.

Makipa wa timu hii nao wanavaa suruali za aina ya pajama kama alizokuwa akivaa Kiraly alipokuwa uwanjani.

Klabu hii inayo uwanja mkubwa, hoteli, kituo cha kulea watoto wa mtaani, vyumba vya mikutano na aina mbalimbali za burudani.

Vile vile ina kituo cha kufundisha soka na michezo mingine kwa chipukizi wapatao 250.

“Nimeanzisha hii klabu kwa sababu siwezi kuwa mbali na mchezo wa soka,” alisema hivi karibuni.

Mara nyingi huenda Uingereza na kutumia muda mrefu katika klabu ya Crystal Palace ambayo mwenyewe anasema ndio iliyompa mapenzi makubwa na kumthamini.

“Nikifika Crystal Palace hujiona nipo nyumbani na hufurahi sana nikikutana na wazee wenzangu niliocheza nao,” aliongeza kipa huyo gwiji.

Wakati fainali za Euro 2024 zikiendelea huko Ujerumani mashabiki wa soka wanasubiri kuona zitawekwa rekodi nyingine ngapi za mashindano haya ambayo yamekuwa yakitoa matokeo yasiyotarajiwa.