Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Guimaraes arudishwa mezani Manchester City

TETESI Pict

Muktasari:

  • Mabosi wa Man City wanataka kuboresha eneo lao la kiungo ambalo limekuwa na upungufu kwa msimu huu hususani baada ya kuumia kwa Rodri na Guimaraes anaonekana kama chaguo lao sahihi.

MANCHESTER City imeonyesha kuwa tayari kuanza tena mazungumzo na Newcastle United kwa ajili ya kumsajili kiungo wao na timu ya taifa ya Brazil, Bruno Guimaraes, mwenye umri wa miaka 27, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Mabosi wa Man City wanataka kuboresha eneo lao la kiungo ambalo limekuwa na upungufu kwa msimu huu hususani baada ya kuumia kwa Rodri na Guimaraes anaonekana kama chaguo lao sahihi.

Mkataba wa Guimaraes unatarajiwa kumalizika mwaka 2028.

 Msimu huu, Bruno  amecheza mechi 39 za michuano yote, amefunga mabao matatu na kutoa asisti nane.

Newcastle inadaiwa kuwa tayari kumuuza fundi huyu lakini inahitaji zaidi ya Euro 100 milioni ili kufanya hivyo, kwani ni miongoni mwa wachezaji wao tegemeo.


Rodrygo

CHELSEA iko tayari kulipa Euro 120 milioni kwenda Real Madrid kwa ajili ya kumsajili winga wao na timu ya taifa ya Brazil, Rodrygo, mwenye umri wa miaka 24, ambaye inamwangalia kama usajili wao mkubwa kwenye dirisha lijalo.

Rodrygo ni miongoni mwa wachezaji tegemeo katika kikosi cha kwanza Madrid, mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2028.


Tijjani Reijnders

KIUNGO wa AC Milan na timu ya taifa ya Uholanzi, Tijjani Reijnders, 26, yupo katika rada za Manchester City ambayo imeandaa ofa isiyopungua Euro 50 milioni kwa ajili ya kukamilisha usajili wake katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Tijjani ni mmoja kati ya wachezaji tegemeo katika kikosi cha Milan na msimu huu amecheza mechi 45 za michuano yote na kufunga mabao 13.


Jarrad Branthwaite

EVERTON ipo tayari kumuuza beki wake wa kati raia wa England, Jarrad Branthwaite, mwenye umri wa miaka 22, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi ambapo vigogo mbalimbali barani Ulaya wameonyesha nia ya kumsajili.

Kati ya timu zinazopewa nafasi kubwa ya kumsajili staa huyu ni Manchester United na Tottenham.


Alexander Isak

ARSENAL na Liverpool zinaangalia uwezekano wa kusajili washambuliaji wengine katika dirisha lijalo baada ya Newcastle United kusisitiza kuwa hawana mpango wa kumsajili straika wa timu hiyo na timu ya taifa ya Sweden, Alexander Isak, 25.

Msimu huu Isak amecheza mechi 35 za michuano yote na kufunga mabao 24. Mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2028.


Yahia Fofana

NEWCASTLE, Wolves na Brentford zinapambana kuiwania saini ya kipa wa Angers na timu ya taifa ya Ivory Coast, Yahia Fofana, 24, ambaye anauzwa kwa kiasi kisichopungua Pauni 15 milioni.

Fofana ambaye ni miongoni mwa makipa tegemeo katika kikosi cha kwanza cha Angers, mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwakani.


Jobe Bellingham

CHELSEA inaongoza vita ya kuiwania saini ya kiungo wa kati wa Sunderland na timu ya taifa ya England ya vijana wenye umri chini ya miaka 21, Jobe Bellingham, 19, ambaye pia anahitajika na Manchester United, Arsenal, Tottenham, Brighton na Crystal Palace.

Msimu huu Jobe amecheza mechi 36 za michuano yote na kufunga mabao manne.


Douglas Luiz

JUVENTUS iko tayari kumuuza kiungo wake wa kati wa kimataifa wa Brazil, Douglas Luiz, 26, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi lakini kwa timu zitakazokuwa tayari kutoa kiasi kisichopungua Euro 40 milioni.

Luiz amekuwa akihusishwa sana na Manchester City. Mkataba wake na Juventus unamalizika mwaka 2029.