Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Amorim anatia huruma Man United

AMORIM Pict

Muktasari:

  • Rekodi ya Amorim katika Ligi Kuu England ni mbaya sana na inaonyesha kuwa ana wastani wa pointi moja kwenye kila mechi tofauti na makocha wengine waliomtangulia.

MANCHESTER, ENGLAND: NDIO hivyo. Baada ya kukiri mwenyewe kwamba yeye ni miongoni mwa makocha wenye rekodi mbovu kuwahi kutokea Manchester United na kusisitiza kwamba anahitaji kushinda Europa League ili kuweka mambo sawa, vitabu vinaonyesha kwamba kocha huyu Mreno ndio ana takwimu mbovu kuliko yeyote tangu kuondoka kwa Sir Alex Ferguson miaka 12 iliyopita.

Rekodi ya Amorim katika Ligi Kuu England ni mbaya sana na inaonyesha kuwa ana wastani wa pointi moja kwenye kila mechi tofauti na makocha wengine waliomtangulia.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 40 amemtetea kipa anayeshutumiwa sana, Andre Onana, kabla ya mechi muhimu ya Alhamisi kwenye uwanja wa Old Trafford.

Tangu Amorim atue, Man United imekusanya pointi 23 tu katika mechi 21 akiwa ameiongoza kushinda mechi sita pekee na vichapo 10.

Man United ilikuwa na tofauti ya pointi nne tu kutoka nafasi ya kufuzu Ligi ya Mabingwa kabla ya Amorim kuwasili lakini sasa tofauti ya alama ni 17.

Man United wapo nafasi ya 14 kwenye msimamo, pointi tatu tu juu ya nafasi ya kushuka daraja na wako pointi 17 nyuma ya majirani zao Manchester City walio nafasi ya tano.

Katika mashindano yote, rekodi ya Amorim ni mbaya hata kuliko ya Rangnick, ambaye alishinda asilimia 37.9 ya mechi zake alipokuwa kocha wa mpito msimu wa 2021/22.

Wawili hao Rangnick na Amorim ndio makocha pekee walioshindwa kuiongoza timu hiyo kupata ushindi wa walau nusu ya mechi walizocheza.

Hata David Moyes, ambaye alidumu kwa msimu mmoja tu baada ya Ferguson kuondoka, alishinda mechi zaidi ya Amorim.

Jose Mourinho, ambaye alidai kumaliza nafasi ya pili na United msimu wa 2017/18 ilikuwa moja ya mafanikio yake makubwa, anaongoza kwa rekodi bora zaidi baada ya Fergie.

Amorim bado yuko mbali kufikia mafanikio ya Mreno mwenzake, Mourinho.

Msimu huu huenda ukawa mbaya zaidi kwa Man United tangu waliposhuka daraja mwaka 1974.

Na hali inazidi kuwa mbaya, kwani wapinzani wao wakuu Liverpool wapo karibu kutwaa taji lao la 20 la ligi, jambo ambalo litawafanya kufikia rekodi ya Man United.

Mashabiki wa Liverpool, licha ya kuwa na furaha, bado hawajasahau kulinganisha hali ya sasa ya Man United na wakati wao wa mateso kipindi timu ipo chini ya Roy Hodgson ambapo inatajwa kuwa moja ya vipindi vigumu kuwahi kutokea kwao.

Hodgson alifukuzwa Januari 2011 baada ya kuchukua nafasi ya Rafael Benitez kwa kushindwa kufikia matarajio na Liverpool ikawa karibu kushuka daraja.

Hata hivyo, alipata pointi 25 katika mechi 20 za Ligi Kuu kabla ya kutimuliwa na jambo baya kwa Amorim ni kwamba hata kocha huyu alikuwa na takwimu nzuri kuliko yeye.