Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

MAAJABU YA MUNICH: PSG, Arsenal historia inawabeba

MUNICH Pict

Muktasari:

  • Tangu mwaka 1993 michuano hii ilipoanza kuitwa Ligi ya Mabingwa Ulaya kutoka Kombe la Ulaya, fainali tano zimepigwa Ujerumani na tatu kati ya hizo zimeshuhudia bingwa akiwa ni ambaye hajawahi kubeba taji hilo.

LONDON, ENGLAND: YANAWEZA yakawa ni maajabu. Ndiyo, kama ni Arsenal au Paris Saint Germain atakayecheza fainali na kubeba taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya utakuwa ni mwendelezo maajabu ya fainali zinazopigwa Ujerumani kutoa bingwa mpya wa michuano hiyo.

Tangu mwaka 1993 michuano hii ilipoanza kuitwa Ligi ya Mabingwa Ulaya kutoka Kombe la Ulaya, fainali tano zimepigwa Ujerumani na tatu kati ya hizo zimeshuhudia bingwa akiwa ni ambaye hajawahi kubeba taji hilo.

Uwezekano wa Arsenal au PSG kushinda taji hilo unatokana na mahali ambako fainali itachezwa huko Munich, Ujerumani.

Miamba hiyo inaweza kuwa na sababu ya kusherehekea kwa sababu mechi zote nne zilizopita ziliendeleza maajabu hayo ya kutoa bingwa mpya ambaye hakuwahi kuchukua taji hilo hapo kabla na mara mbili mabingwa walitokea England.

Ujerumani imeandaa fainali nane kabla na hii ni ya tisa katika majiji na viwanja tofauti tangu mwaka 1959 na mwaka huu 2025 zinaandaliwa Allianz Arena.

Allianz Arena ni moja ya viwanja vilivyotoa bingwa mpya wa michuano hiyo mwaka 2012 na Chelsea ilibeba mbele ya Bayern Munich ilipoichapa kwa mikwaju 4-3 baada ya sare ya bao 1-1 muda wa kawaida na niongeza.

Fainali nyingine ni ile ya kwanza mwaka 1979 iliyozikutanisha Nottingham Forest dhidi ya Malmo ya Sweden na Forest ilishinda 1-0.

Matokeo kama hayo ya 1-0 yalijirudia katika fainali ya 1993 wakati Marseille ya Ufaransa ilipoichapa AC Milan na kushinda taji lao pekee la Ligi ya Mabingwa.

Borussia Dortmund ilikuwa timu ya kwanza kutoka nchi mwenyeji kunufaika na historia hiyo ya bahati iliposhinda 3-1 dhidi ya Juventus mwaka 1997.

Hadi sasa imeshuhudiwa mabingwa 15 wa michuano hiyo mikubwa Ulaya.

Ujerumani imeandaa fainali hizo mara nne katika Jiji la Munich, katika viwanja vya Olympiastadion mara tatu na Allianz Arena mara moja kabla ya mwaka huu kuandaa tena.

Katika Jiji la Munich ambalo ndilo linaandaa fainali ya mwaka huu linazisubiri kati ya Arsenal au PSG zitakazokutana Aprili 29, na kati ya Barcelona au Inter Milan zitakazokutana Aprili 30.

Hii ina maana mmoja kati ya Arsenal na PSG ambazo hazijawahi kubeba taji hilo, itacheza fainali na Inter iliyolibeba mara tatu au Barcelona ililolibeba mara tano.

Arsenal ilitinga nusu fainali kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2009, baada ya kuitoa mabingwa wa kihistoria wa michuano hiyo Real Madrid yenye mataji 15, kwa jumla ya mabao 5-1, huku PSG ikiitoa Aston Villa kwa mabao 5-4 na inatabiriwa kushinda taji hilo kutokana na historia iliyopo ya fainali kuchezwa katika jiji hilo la Munich.

PSG imefika fainali mara moja na kupoteza bao 1-0 kutoka kwa Bayern Munich mwaka 2020.

Akizungumzia nafasi ya timu yake kushinda taji hilo kwa mara ya kwanza, Kocha Mikel Arteta alisema: “Hivyo jinsi tunavyowaza, unaweza ukaona hata wachezaji wanavyoonyesha utayari kwamba wanaweza kushinda na yeyote. Sasa tunapaswa kuendelea na fikra hizo hivyo kwa sababu naamini tuna kasi na tuna njaa na dhamira.”