Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Haaland aweka rekodi nyingine

HAALAND Pict

Muktasari:

  • Haaland alifikia rekodi hiyo baada ya kufunga penalti katika dakika ya 11 ya mchezo dhidi ya Brighton, akifikisha mabao 84 ya ligi tangu ajiunge na Man City akitokea Borussia Dortmund mwaka 2022.

MANCHESTER, ENGLAND: NYOTA wa Manchester City, Erling Haaland ameweka rekodi mpya ya kuhusika katika mabao 100 kabla ya kufikisha mechi 100 katika Ligi Kuu Enngland akiivuka ya nyota wa zamani wa Newcastle United na timu ya taifa ya England, Alan Shearer.

Bao moja la penalti dakika ya 11 kati ya mawili ya Man City dhidi ya Brighton katika sare ya mabao 2-2 kwenye Uwanja wa Etihad, yalimfanya Haaland afikishe mabao 84 na asisti 16, katika michezo 94, akimzidi Shearer aliyehusika na mabao 100 akifunga 79 na kuasisti 21 katika mchezo wa 100 mwaka 1994.  

Staa wa Liverpool, Mohamed Salah na nyota wa zamani wa Manchester United, Eric Cantona wenyewe walihusika  katika mabao 100 baada ya michezo 116.

Licha ya Haaland kuisaidia timu yake kuanza vyema katika mchezo huo, Man City ilipoteza pointi nyumbani kwa mara ya sita msimu huu baada ya sare ya mabao 2-2.

Akizungumza na BBC 'Match of the Day' baada ya mchezo huo, Kocha wa Man City, Pep Guardiola alisema: "Ulikuwa ni mchezo mzuri. Mchezo mgumu. Najua jinsi ilivyokuwa ngumu kufika katika hali tuliyonayo sasa. Wachezaji walijitolea kila kitu. Hakuna namna inabidi tuchukue pointi na kuendelea mbele. Bila shaka, nina imani na kila wakati nina imani. Wachezaji walicheza vizuri. Watetezi wote walikuwa bora. Tulikuwa karibu kupata matokeo, lakini kwa bahati mbaya hatukuweza."