Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Inzaghi atua rasmi Al Hilal, akiitosa Inter Milan

INZAGHI Pict

Muktasari:

  • Kocha huyo wa Italia amejiunga na klabu hiyo uinayoshiriki Ligi Kuu ya Saudia (Saudi Pro League) kwa mkataba wa miaka miwili baada ya kuondoka Inter juzi Jumanne.

Simone Inzaghi ametangazwa kuwa kocha mkuu wa klabu ya Al-Hilal ya Saudi Arabia, siku moja baada ya kuondoka Inter Milan ya Italia ikitosa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya mbele ya PSG ya Ufaransa.

Kocha huyo wa Italia amejiunga na klabu hiyo uinayoshiriki Ligi Kuu ya Saudia (Saudi Pro League) kwa mkataba wa miaka miwili baada ya kuondoka Inter juzi Jumanne.

Klabu hiyo ya Serie A ilipoteza kwa mabao 5-0 katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Jumamosi (Mei 31) dhidi ya Paris St-Germain.

Inzaghi ameiongoza Inter Milan tangu mwaka 2021, akiipa taji la Ligi Kuu, Serie A 2023-24 na kushinda Coppa Italia mara mbili.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 49 pia aliiongoza Inter hadi fainali ya Ligi ya Mabingwa 2023, ambapo walifungwa 1-0 na Manchester City.

Inzaghi anarithi mikoba ya kocha wa Ureno Jorge Jesus, ambaye aliiongoza Al-Hilal kutwaa taji la Saudi Pro League msimu wa 2023-24, lakini alitimuliwa mwezi uliopita baada ya timu hiyo kutolewa hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Asia.

Vyombo vya habari vya Italia vimeripoti kuwa mkataba wa Inzaghi una thamani ya hadi Euro 30 milioni kwa mwaka.

Jukumu lake la kwanza litakuwa kutwaa ubingwa wa Kombe la Dunia la Klabu 2025 zinazofanyikia Marekani, ambapo Al-Hilal watamenyana na Real Madrid katika mchezo wa ufunguzi utakaofanyika Miami 18 Juni.