Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kane atajwa chambo kwa Gordon

Muktasari:

  • Tangu kuwasili kwao, wachezaji hao wamekuwa na mchango mkubwa, ambapo wamehusika katika jumla ya mabao 94, hiyo ni rekodi mpya katika Bundesliga tangu mwaka 1988.

MUNICH, UJERUMANI: KLABU ya Bayern Munich, imeendelea kuvuna vipaji kutoka Ligi Kuu England katika miaka ya hivi karibuni huku nyota kama Harry Kane, Michael Olise na Luis Diaz wakihamia Ligi Kuu Ujerumani na kufanya vizuri.

Tangu kuwasili kwao, wachezaji hao wamekuwa na mchango mkubwa, ambapo wamehusika katika jumla ya mabao 94, hiyo ni rekodi mpya katika Bundesliga tangu mwaka 1988.

Sasa taarifa kutoka Ujerumani zinaeleza kuwa, Kane anaweza kuwa na mchango mkubwa katika kumshawishi mchezaji mwenzake wa timu ya taifa ya England, Anthony Gordon, kujiunga na miamba hiyo ya Bundesliga mwishoni mwa msimu.

Gordon ambaye anaichezea Newcastle United, ameivutia Bayern kutokana na uwezo wake wa kucheza nafasi tofauti za ushambuliaji, ikiwemo kubadilika kutoka winga hadi mshambuliaji wa kati katika baadhi ya mechi msimu huu.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25, aliwahi kuhusishwa kujiunga na Liverpool mwaka 2024, lakini dili hilo halikukamilika. Baadaye alisaini mkataba mpya na Newcastle unaodumu hadi 2030.

Inaelezwa kuwa, tayari Gordon amewasiliana na Kane kuhusu uwezekano huo huku wachambuzi wakiamini kuwa uwepo wa Kane unaweza kuwa kivutio kikubwa kwa wachezaji wa England kujiunga na klabu hiyo ya Ujerumani.

Hata hivyo, kikwazo kikubwa kinabaki kuwa thamani ya mchezaji huyo, ambapo Newcastle wanadaiwa kuhitaji kiasi cha pauni 75 milioni ili kumuachia.