Klabu za England zinapambana kumpata Riccardo Calafiori

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa tovuti ya Express, timu yoyote itakayohitaji kukamilisha dili la staa huyu italazimika kulipa kiasi kisichopungua Pauni 40 milioni kama ada ya uhamisho.

LIVERPOOL, Arsenal, Chelsea na West Ham zote zimeonyesha nia ya kumsajili beki kisiki wa Bologna na Italia, Riccardo Calafiori katika dirisha hili.

Kwa mujibu wa tovuti ya Express, timu yoyote itakayohitaji kukamilisha dili la staa huyu italazimika kulipa kiasi kisichopungua Pauni 40 milioni kama ada ya uhamisho.

Staa huyu amewasha pia kwenye Euro 2024.


BRIGHTON imebaki njia panda juu ya usajili wa kiungo wa Leicester City, Kiernan Dewsbury-Hall, 25, baada ya kuibuka kwa taarifa kwamba Chelsea imefikia makubaliano ya kumsajili staa huyo katika dirisha hili. Mabosi wa Brighton hawaelewi kwa sababu walishafanya makubaliano na staa huyo na walishamfanyia hadi vipimo vya afya.


Newcastle inajaribu kuzunguma na wawakilishi wa kipa wa Notrtingham Forest, Odysseas Vlachodimos, 30, ili kuipata saini yake katika dirisha hili.

Mabosi wa Newcastle wanataka kumtumia kiungo wao Elliot Anderson kama sehemu ya ofa ya kuipata huduma ya fundi huyo.


BAADHI ya viongozi wa juu wa Barcelona wameripotiwa kutokubaliana na mpango wa timu hiyo kutaka kumsajili winga wa Athletic Bilbao, Nico Williams ambaye ameonyesha kiwango bora akiwa na timu yake kwa msimu uliopita, pia na timu ya taifa ya Hispania katika michuano ya Euro inayoendelea huko Ujerumani. Mkataba wake na Bilbao unamalizika mwaka 2027.


LEICESTER City ipo katika hatua za mwisho kumsajili kiungo wa Chelsea, Michael Golding katika dirisha hili baada ya kufikia makubaliano na mabosi hao wa London wiki iliyopita. Staa huyu mkataba wake unamalizika mwaka 2025. Kiwango chake akiwa na timu za vijana za Chelsea kwa msimu uliopita, kimesababisha timu mbalimbali kuonyesha nia ya kutaka kumsajili.


LEICESTER City ipo katika hatua za mwisho kumsajili kiungo wa Chelsea, Michael Golding katika dirisha hili baada ya kufikia makubaliano na mabosi hao wa London wiki iliyopita. Staa huyu mkataba wake unamalizika mwaka 2025. Kiwango chake akiwa na timu za vijana za Chelsea kwa msimu uliopita, kimesababisha timu mbalimbali kuonyesha nia ya kutaka kumsajili.


MANCHESTER United imepanga kuachana na beki wa Barcelona na Uruguay, Ronald Araujo, 25, baada ya kutajiwa kiasi kikubwa cha pesa na mchezaji kutoonysha nia ya kutaka kuondoka kwa sasa.

Mkataba wa sasa wa Araujo unatarajiwa kumalizika mwaka 2026. Msimu uliopita alicheza mechi 37 za michuano yote.