Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kumbe Harry Maguire amebadili jina buana!

MAGUERE Pict

Muktasari:

  • Maguire, 32, aliibukia kwenye soka tangu 2011 wakati akiwa na kikosi cha Sheffield United kabla ya kuhamia Hull City, Leicester City na sasa Manchester United, iliyomsaini kwa ada ya Pauni 85 milioni mwaka 2019.

LONDON, ENGLAND: BEKI, Harry Maguire amefichua kwamba wakati anazaliwa jina lake lilikuwa jingine kabisa, lakini alilazimika kulibadilisha kwa sababu ya kushangaza.

Maguire, 32, aliibukia kwenye soka tangu 2011 wakati akiwa na kikosi cha Sheffield United kabla ya kuhamia Hull City, Leicester City na sasa Manchester United, iliyomsaini kwa ada ya Pauni 85 milioni mwaka 2019.

Beki huyo wa kati maisha yake ya soka la timu za wakubwa yalianzia Sheffield wakati alipokuwa na umri wa miaka 18, wakati ambao ndio uliomfanya abadili jina lake.

Staa huyo wa England wakati anazaliwa alipewa jina la Jacob Harry Maguire, lakini mama yake alibadili mawazo baada ya kufikisha umri wa miezi mitatu tu.

Na hiyo iliyokana na kila mtu kuanza kumwita kwa jina la ‘Jakey’, ambalo mama yake hakulipenda. Hivyo, aliamua kuyabadili majina hayo, badala ya kuitwa Jacob Harry, aliamua kumwita kwa jina la Harry Jacob, lakini hakulitumia hadi alipopata hati yake ya kusafiria alipofikisha umri wa miaka 18.

Maguire alisema: “Mama yangu alinipa jina la Jacob Harry (Maguire) nilipozaliwa. Kisha miezi mitatu baadaye, watu wakaanza kuniita Jakey.

“Hakupenda, hivyo aliamua kulibadili mbele nyuma na kuitwa Harry Jacob. Lakini, hakuweza kulifanya kuwa rasmi hadi hapo nilipofika umri wa miaka 18. Nilipotimiza tu umri wa miaka 18 nilibadili jina na sasa rasmi naitwa Harry Jacob.”

Maguire amefunga mabao 17 na asisti tisa katika mechi 255 alizochezoea Man United tangu alipojiunga na timu hiyo miaka sita iliyopita. Beki huyo wa kati amefunga mara saba pia katika mechi 64 alizochezea timu ya taifa ya England.