Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kwa Lewandowski, hata Ronaldo, Messi hawana

HAWANA Pict

Muktasari:

  • Mshambuliaji huyo mzoefu alifunga mabao mawili dhidi ya waajiri wake wa zamani Borussia Dortmund katika ushindi wa 4-0 katika mchezo wa robo fainali uliopigwa kwenye dimba la  Estadi Olimpic Lluis Companys.

BARCELONA, HISPANIA: MSHAMBULIAJI wa Barcelona, Robert Lewandowski aliweka rekodi mpya katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ambayo hata Lionel Messi na Cristiano Ronaldo hawana.

Mshambuliaji huyo mzoefu alifunga mabao mawili dhidi ya waajiri wake wa zamani Borussia Dortmund katika ushindi wa 4-0 katika mchezo wa robo fainali uliopigwa kwenye dimba la  Estadi Olimpic Lluis Companys.

Lewandowski alifunga bao lake la 10 na 11 katika mashindano ya Ulaya msimu huu dakika ya 48 na 66 dhidi ya wababe hao kutoka Ujerumani.

Kwa kufanya hivyo, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 36 amekuwa mchezaji wa kwanza kufunga angalau mabao 10 katika msimu mmoja wa Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na timu tatu tofauti.

Lewandowski alifunga mabao 10 akiwa na Dortmund katika msimu wa 2012/13, kabla ya kufanya hivyo pia akiwa na Bayern Munich msimu wa 2019/20 na 2021/22.

Katika mwaka wake wa tatu akiwa Barcelona, pia amefanya hivyo na ameshafunga mabao 11.

Rekodi hii haikufikiwa hata na Ronaldo ambaye alifunga mabao 10 au zaidi mara mbili tu akiwa Real Madrid licha ya kucheza pia michuano hiyo akiwa na Manchester United na Juventus.

Lewandowski sasa ana mabao 40 msimu huu katika mashindano yote, pungufu ya bao moja kufikisha mia moja akicheza Hispania.

Jambo la kushangaza ni nyota huyo wa kimataifa wa Poland, amefunga mabao mengi zaidi dhidi ya Dortmund kuliko timu yoyote nyingine katika michuano ya Ulaya, kitendo kinachowaumiza mashabiki wa timu hiyo waliomshabikia sana wakati akiwa nao kwa misimu miwili alipojiunga nao 2010 hadi 2014.

Mbali ya Lewandoski, Raphinha naye juzi aliifikia rekodi ya Lionel Messi ya msimu wa 2011/12 ya kuhusika katika mabao 19 ya michuano hiyo ndani ya msimu mmoja na amefikisha mabao 12 na kutoa asisti saba, wakati Messi alifunga mabao 14 na kutoa asiti tano.

Raphinha atakuwa na nafasi ya kuivuka kabisa rekodi hiyo ikiwa atatoa asisti au kufunga wiki ijayo katika mchezo wa marudiano kati yao na Dortmund utakaopigwa Ujerumani katika dimba la Signal Iduna Park.