Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mashabiki Chelsea wambadilikia Todd Boehly

CHELSEA Pict

Muktasari:

  • Bilionea huyo kutoka Marekani aliongoza ununuzi wa timu hiyo kwa Pauni 4.25 bilioni kutoka kwa Roman Abramovich mwaka 2022. 

LONDON, ENGLAND: MASHABIKI wa Chelsea wameiomba mamlaka inayosimamia Ligi Kuu England kumchunguza mmiliki wao Todd Boehly kutokana na uhusiano wake na kampuni inayouza tiketi za mechi mbalimbali za ligi hiyo.

Bilionea huyo kutoka Marekani aliongoza ununuzi wa timu hiyo kwa Pauni 4.25 bilioni kutoka kwa Roman Abramovich mwaka 2022. 

Tangu wakati huo, amekwenda kwenye harakati ya usajili wa kushangaza, akitumia zaidi ya Pauni 1.2 bilioni kununua wachezaji wapya. 

Boehly, mwenye umri wa miaka 51, na kampuni yake ya  Clearlake Capital na BlueCo zinazomiliki hisa katika timu hizo zimepokea upinzani mkali kutoka kwa kundi la mashabiki la Chelsea liitwalo Chelsea Supporters’ Trust.

Kundi hilo lilituma barua kwa mkurugenzi mtendaji wa EPL, Richard Masters kutokana na uhusiano wa Boehly na kampuni ya uuzaji wa tiketi ya Vivid Seats. 

Tangu kuwekeza mwaka 2021, Boehly amekuwa mkurugenzi katika biashara hii inayouza tiketi za mechi za EPL, ikiwa ni pamoja na mechi za Chelsea, kwa bei za juu sana, mara nyingi zaidi ya maelfu ya pauni juu ya thamani halisi. 

Kampuni hiyo ya Marekani imeorodheshwa na EPL  kama “tovuti isiyoidhinishwa ya uuzaji wa tiketi” na inaelekeza mashabiki “kuwa na tahadhari kubwa” juu yao.

Tiketi za mechi ya London derby kati ya Chelsea na Tottenham itakayopigwa Stamford Bridge Aprili 3, zinapatikana kwa zaidi ya Pauni 2,000.

Kwa mechi dhidi ya Liverpool dhidi ya Chelsea itakayopigwa Mei 2, kupitia tovuti hiyo inauzwa kwa Pauni 3,200 kutoka Pauni 442 ambayo ni bei yake halisi.

Barua hiyo pia inalalamikia hali ya viongozi wa timu hiyo katika kupambana na wauzaji haramu wa tiketi nje ya uwanja katika siku za mechi. 

Barua hiyo inaeleza: “Uhusiano wa Boehly na Vivid Seats ni mbaya kabisa na unadhoofisha juhudi za Chelsea FC, EPL, na Polisi katika kupambana na uuzaji wa tiketi haramu. Vivid Seats inaendelea kuuza tiketi kwa bei za juu kuliko ile ya halali. Tunaamini sasa ni wakati wa mamlaka kuchukua hatua haraka na kuhakikisha kwamba mmiliki mkuu wa klabu yetu  anaachana kuhamasisha uuzaji wa tiketi kwa bei ya juu kuliko ile ya halali.”