Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mke wa kocha Man United asimuliwa alivyotimuliwa

Muktasari:

  • Kocha huyo mkongwe wa Uholanzi aliyetamba na Ajax, Barcelona na Bayern Munich alitua Old Trafford 2014 kuchukua mikoba ya David Moyes na kuondoka miaka miwili baadaye akiwa na ubingwa wa Kombe la FA, lakini moyo wake ukiwa uliovunjika.

AMSTERDAM, UHOLANZI: LICHA ya mafanikio makubwa akiwa na klabu kubwa Ulaya, Louis van Gaal hajawahi kuvunjwa moyo kama ilivyotokea alipokuwa kocha wa Manchester United.

Kocha huyo mkongwe wa Uholanzi aliyetamba na Ajax, Barcelona na Bayern Munich alitua Old Trafford 2014 kuchukua mikoba ya David Moyes na kuondoka miaka miwili baadaye akiwa na ubingwa wa Kombe la FA, lakini moyo wake ukiwa uliovunjika.

Mkewe, Truus van Gaal amesimulia jinsi alivyohisi kufukuzwa kwake kulikotokea ghafla na bila heshima ambapo akizungumza kupitia filamu ya maisha ya Van Gaal, alisema:

“Nilijua Louis atafukuzwa Manchester United, nilihisi tu.”

Aliongeza: “Tulikuwa na chumba chetu pale kilichojaa furaha, tukila chakula kizuri na kushirikiana na magwiji kama (Alex) Ferguson na Bobby Charlton. Lakini ghafla, waliacha kutusalimia, walikuwa tu wanapunga mkono kwa mbali. Nilisema, ‘Louis, utatimuliwa. Tambua hilo.’”

Van Gaal aliendelea na kazi yake licha ya uvumi kwamba Jose Mourinho alikuwa akisubirishwa kurithi mikoba yake na alibeba ubingwa wa FA 2016 dhidi ya Crystal Palace, lakini kumaliza ligi akiwa nafasi ya tano na kukosa nafasi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kulitosha kumtimua.

“Baada ya fainali ya FA, Louis aliniambia ‘tumefanikiwa!’ Nikamwambia lakini wanadai umefukuzwa. Akakasirika sana, ‘mbona unaharibu sherehe yangu? Acha maneno hayo.”

Baadaye, Van Gaal akiwa kazini aliafiki kauli ya mkewe alipompigia simu mkewe kwa sauti iliyovunjika moyo na kumsalimia. “Hujambo. Unaweza kurudi nyumbani, ulikuwa sahihi (kwamba nimefukuzwa).Nilipofika (nyumbani) niliweza kuona kwamba alikuwa amelia. Nilimkumbatia, nami pia nililia,” alisema Truus.