Nyuma ya vita ya ubingwa Ufaransa
Muktasari:
- Zikiwa zimesalia raundi tano, PSG wanaongoza Ligue 1 kwa tofauti ya pointi nne dhidi ya Lens, ambao watakutana nao katika mchezo wa pili kutoka mwisho wa msimu. “Hii ni ligi ngumu, lakini hatujawahi kuwa na mpinzani kama huyu miaka mingine,” anaongeza beki huyo wa kimataifa wa Brazil.
PARIS, UFARANSA: TAYARI bingwa wa Ligi Kuu Ujerumani (Bundesliga) ameshafahamika, Bayern Munich, lakini timu katika ligi zingine zinaendelea kupambana kusaka ubingwa na lolote linaweza kutokea kati ya sasa mwisho wa msimu kule Italia (Serie A), Hispania (La Liga), England (EPL) na Ufaransa (Ligue 1).
Hata hivyo, Paris Saint-Germain (PSG) wana nafasi kubwa katika mbio za kutetea ubingwa wa Ligue 1, lakini wanakabiliwa na ratiba ngumu ya mechi saba ndani ya siku 23.
“Ubingwa bado uko wazi. Lens hawajakubali kushindwa,” anasema nahodha wa PSG, Marquinhos, baada ya timu ya ushindi wao rahisi wa mabao 3-0 dhidi ya Nantes wiki hii. Nantes walionyesha upinzani mwanzoni mwa mchezo, na hata walipofunga bao ambalo lingeweza kuwa la kusawazisha, lakini likakataliwa kwa kuotea kabla ya hatimaye kukubali kipigo katika Uwanja wa Parc des Princes.
Zikiwa zimesalia raundi tano, PSG wanaongoza Ligue 1 kwa tofauti ya pointi nne dhidi ya Lens, ambao watakutana nao katika mchezo wa pili kutoka mwisho wa msimu. “Hii ni ligi ngumu, lakini hatujawahi kuwa na mpinzani kama huyu miaka mingine,” anaongeza beki huyo wa kimataifa wa Brazil.
“Lens wana msimu mzuri sana. Hii ni nzuri kwetu. Inatulazimisha kufanya kazi kwa bidii na kubaki makini hadi mwisho wa msimu. Hatuna muda wa kupumzika. Tutakuwa tunacheza kila baada ya siku tatu.”
Khvicha Kvaratskhelia aliyeifungia PSG mabao mawili huku lingine likifungwa na Desire Doue, anasema wanafikiria zaidi kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao. Mchezaji huyo wa Georgia, ambaye sasa ana mabao 16 msimu huu, amekuwa muhimu zaidi kwa PSG kipindi hiki cha mwisho wa msimu.
Ratiba ngumu ya PSG imejiletea yenyewe, kwani baadhi ya mechi za ligi ziliahirishwa ili kujiandaa na michezo ya Ligi ya Mabingwa, jambo ambalo lilikosolewa na Lens.
Hata hivyo, baada ya kuahirisha mechi hizo, PSG sasa wanakabiliwa na mwezi wa mwisho wenye kasi kubwa ya michezo, ambao ungekuwa mbaya zaidi kama wasingeondolewa kwenye Coupe de France na Paris FC mwezi Januari.
Kama anavyoeleza Luis Enrique, kocha wa timu hiyo, wachezaji wake wako katikati ya ratiba ya mechi tisa ndani ya siku 28, na nafasi ya mastaa Kvaratskhelia, Desire Doue na Ousmane Dembele kuanza pamoja katika mechi zote hizo ni ndogo.
Kutokana na shinikizo kutoka kwa Lens, PSG wamekuwa wakitegemea zaidi wachezaji wao wa kawaida. Usajili pekee mwezi Januari ulikuwa kiungo mwenye miaka 18 Dro Fernandez kutoka Barcelona.
Wachezaji chipukizi waliotokea katika akademi mwanzoni mwa msimu wamekuwa pembeni tangu wakati huo. Ibrahim Mbaye amecheza dakika chache katika miezi miwili iliyopita; Quentin Ndjantou hajacheza tangu mwanzo wa mwaka kutokana na jeraha la misuli ya paja na Senny Mayulu amekuwa akisumbuliwa na jeraha la mguu.
Ni Warren Zaire-Emery pekee ndiye ameendelea kuanza mara kwa mara na hata akicheza kama beki wa kushoto dhidi ya Nantes.
PSG wana ratiba nafuu zaidi ukilinganisha na Lens, wakianza na safari ya kwenda kucheza na Angers leo Jumamosi, lakini michezo miwili dhidi ya Bayern Munich itawachosha.
Mara ya mwisho walipokuwa na mechi ya ligi kati ya michezo ya Ligi ya Mabingwa ilikuwa dhidi ya Monaco mwezi Februari, ambapo baadaye waliwashinda PSG kwenye ligi.
Lens bado hawajatoka kwenye mbio za ubingwa, ingawa unaweza kuanza kuwatoroka iwapo wangepoteza jana, lakini wako karibu kuandika historia.
Waliishinda Toulouse kwa mabao 4-1 na kufuzu fainali ya kwanza ya Coupe de France baada ya miaka 28. Filimbi ya mwisho katika Uwanja wa Stade Bollaert-Delelis ilishuhudia mashabiki wakivamia uwanja kwa furaha.
Kikosi hicho cha kocha Pierre Sage kilionyesha kiwango kinachostahili hadhi mpya kama timu ya pili bora nchini Ufaransa, huku straika Florian Thauvin akihusika katika mabao yote manne. Ikiwa watakosa ubingwa wa ligi, kushinda Coupe de France kwa mara ya kwanza kutakuwa faraja kubwa kwao.
Nice, ambao wako karibu na eneo la kushuka daraja pia wana nafasi ya kuokoka katika msimu wao baada ya kuifunga Strasbourg katika nusu fainali nyingine ya kombe la ligi. Claude Puel, ambaye alijiunga katikati ya msimu kama kocha wa muda anaweza kuondoka akiwa na taji lisilotarajiwa.