Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Orlando Magic ni mwaka wao?

Muktasari:

  • Nyota wa timu hiyo Paolo Banchero, Franz Wagner na Jalen Suggs waliumia msimu huu wakiwa wamcheza pamoja kwenye mechi sita kwa dakika 97 kabla ya Suggs kupata tena jeraha, safari hii ni kuchanika kwa nyama laini za goti na kulazimika kufanyiwa upasuaji.

FLORIDA, MAREKANI: KOCHA wa Orlando Magic, Jamahl Mosley amekuwa kwenye NBA miaka 20, lakini hajawahi kushuhudia msimu wa ajabu kama huu ambao wachezaji, benchi la ufundi na wafanyakazi wa Magic wamepitia.

Nyota wa timu hiyo Paolo Banchero, Franz Wagner na Jalen Suggs waliumia msimu huu wakiwa wamcheza pamoja kwenye mechi sita kwa dakika 97 kabla ya Suggs kupata tena jeraha, safari hii ni kuchanika kwa nyama laini za goti na kulazimika kufanyiwa upasuaji.

Mchezaji mwingine aliyeng’ara, Moe Wagner, aliyekuwa akitajwa kwenye mbio za Mchezaji Bora wa Akiba (Sixth Man of the Year) naye aliumia msuli wa goti  Desemba na kumaliza msimu mapema.

“Ni msimu wa ajabu sana,” anasema Mosley.

“Maumivu ya wachezaji mwanzoni kabisa mwa msimu yalibadilisha namna tunavyopanga na kuchambua mambo. Kwa kweli, naweza kusema msimu huu ulikuwa kama misimu saba ndani ya mmoja.

“Unamkosa Paolo, lazima ubadilike. Franz naye anaumia, unarekebisha tena. Jalen anapotea, unarekebisha. Moe naye anaumia, unarekebisha. Halafu hakuna uhakika wa ni lini wachezaji watarudi. Hayo yote yameathiri namna tunavyowaandaa na kuendesha timu kila siku. Wachezaji wakubwa walikuwa ndani na nje ya kikosi, hali iliyotufanya tuwe na changamoto za kimfumo na kisaikolojia.”


SEHEMU MPYA YA SAFARI

Jumanne usiku, Orlando Magic (41-41) walikutana na Atlanta Hawks (40-42) kwenye mchezo wa kwanza wa play-in wa Kanda ya Mashariki na kuibuka na ushindi  wa 120-95 ambao umewafanya kukutana na Boston Celtics, mabingwa watetezi wa NBA kwenye hatua ya kwanza ya mtoano (play offs). Timu itakayopoteza itakuwa na nafasi moja ya mwisho, kwa kucheza Ijumaa dhidi ya mshindi wa mchezo kati ya Chicago Bulls na Miami Heat.

Ingawa wachezaji wa Magic watapenda kusonga mbele hadi hatua ya kwanza ya mtoano, walikuwa na matarajio makubwa zaidi msimu huu kuliko kupenya kupitia Play-In.

Msimu uliopita, walimaliza nafasi ya tano Mashariki baada ya ushindi wa mechi 47, na waliisumbua Cleveland Cavaliers kwenye raundi ya kwanza hadi mchezo wa saba.

“Ni kweli tulikuwa kwenye mkondo wa mafanikio, na nafikiri msimu huu ndio mara ya kwanza tulihisi presha,” anasema Wagner. “Lakini hiyo ni sehemu ya safari ya maendeleo. Maumivu ya wachezaji yalikuwa changamoto kubwa, lakini tunajivunia umoja wetu. Hilo linaweza kutusaidia siku zijazo.”

Katika mfululizo wa mechi za mtoano dhidi ya Cavs mwaka jana, Magic walifanikiwa asilimia 33 tu ya mashuti yao ya mbali, baada ya Cavs kufunga njia ya painti na kuwaacha wajaribu kuwapiga kwa mashuti ya mbali.

Katika majira ya joto, Magic walimsaini Kentavious Caldwell-Pope kwa mkataba wa miaka mitatu wenye thamani ya Dola 66 milioni wakitarajia ataisaidia kwa mitupo ya mbali na kuachia nafasi za kupenyeza mipira kwa Banchero na Wagner.  Lakini kwa muda mrefu, Caldwell-Pope hakufanya vizuri alikuwa anapiga kwa asilimia 31 tu kabla ya All-Star. Hata hivyo, baada ya mapumziko kidogo, ameanza kuwa moto, akifunga kwa asilimia 44 ya mashuti yake kwenye mechi 3.5 kwa wastani. Katika ushindi dhidi ya Atlanta wiki iliyopita, alifunga pointi 15 kwa mashuti matatu kati ya sita kutoka mbali. “Akiwa kwenye kiwango hicho, mambo huwa rahisi zaidi,” anasema Banchero.