Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Pep Guardiola afunguka ishu ya De Bruyne

PEP Pict (1)
PEP Pict (1)

Muktasari:

  • Kiungo huyu alitangaza Ijumaa kuwa ataondoka Etihad katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi baada ya kuwahudumia Citizens kwa miaka 10 ya mafanikio.

MANCHESTER, ENGLAND: PEP GUARDIOLA amethibitisha ilikuwa ni uamuzi wake kumaliza safari ya kiungo wa klabu hiyo na Ubelgiji, Kevin De Bruyne.

Kiungo huyu alitangaza Ijumaa kuwa ataondoka Etihad katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi baada ya kuwahudumia Citizens kwa miaka 10 ya mafanikio.

Awali, staa huyu alihitaji kuendelea kusalia kwenye viunga hivyo kwa sababu familia yake imeshazoea maisha ya Jiji la Manchester licha ya hapo kuhusishwa na timu mbalimbali barani Ulaya lakini Guardiola aliamua asiongezwe mkataba kwa sababu ya hali yake ya majeraha ambayo kocha huyo anaamini inachangia kupunguza kiwango chake.

"Mimi na klabu tulilazimika kuchukua uamuzi. Si rahisi kwani amekuwa bora sana, mimi, Txiki Begiristain na klabu tulifanya uamuzi na hivyo ndivyo ilivyo. Klabu inabidi iendelee mbele, isonge mbele. Kufikia alichokifanya itakuwa ni vigumu sana. Kusema kwaheri kwa wachezaji hawa ni vigumu sana. Unaweza tu kuwa na shukrani. Klabu ilimpa kila kitu na yeye alitupa kila kitu. Nashukuru sana na nina huzuni kwamba tutaachana baada ya miezi miwili," alisema Guardiola.

"Yeye ndiye mchezaji pekee ambaye atamaliza mkataba wake. Wengine wapo chini ya mikataba lakini bado kuna mambo mengi ambayo klabu na mimi hatujafanya uamuzi juu yake."

Mbali ya De Bruyne, kumekuwa na tetesi kwamba John Stones, Nathan Ake na Manuel Akanji nao ni miongoni mwa wachezaji wengine ambao wanaweza kuondoka katika kikosi hicho kwa msimu ujao.

Guardiola anatarajiwa kufanya usajili wa zaidi ya wachzaji watatu katika dirisha lijalo ambapo atatumia zaidi ya Pauni 170 milioni kiasi kama ambacho walitumia Januari mwaka jana.