Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Viktor Gyokeres anaitaka Arsenal, Chelsea yatoa macho

Muktasari:

  • Gyokeres ametikisa msimu huu akifunga mabao 47 katika mechi 46 — 34 katika ligi, 6 katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, 3 katika Kombe la Ureno na 4 katika Kombe la Ligi. Kiujumla, kwa klabu na timu yake ya taifa, amefunga mabao 56 katika mechi 52. Ukijumlisha na asisti zake 14, Gyoketres amehusika katika mabao 70 katika mechi 52 za michuano yote.

CHELSEA inavutiwa kumsajili mshambuliaji wa Sporting, Viktor Gyokeres, mwenye umri wa miaka 26, lakini staa huyo wa kimataifa wa Sweden anapendelea kutua kwa mahasimu wa London, Arsenal.

Gyokeres ametikisa msimu huu akifunga mabao 47 katika mechi 46 — 34 katika ligi, 6 katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, 3 katika Kombe la Ureno na 4 katika Kombe la Ligi. Kiujumla, kwa klabu na timu yake ya taifa, amefunga mabao 56 katika mechi 52. Ukijumlisha na asisti zake 14, Gyoketres amehusika katika mabao 70 katika mechi 52 za michuano yote.

Licha ya kucheza katika ligi isiyo mojawapo ya tano bora barani Ulaya, anakubalika kama mmoja wa washambuliaji bora duniani akifunga atakavyo na hivyo kuwa gumzo Ulaya nzima.

Arsenal tayari wanapanga mashambulizi sokoni. Tayari imeripotiwa kuwa wana bajeti ya euro 234 milioni kwa ajili ya kusajili wachezaji watatu katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi, na nyota huyo wa Sporting yupo kwenye orodha. Pia Gunners wanawalenga Martin Zubimendi kutoka Real Sociedad na Nico Williams wa Athletic Bilbao. Ingawa Alexander Isak wa Newcastle pia yupo kwenye rada yao, Gyokeres anaonekana kama chaguo nafuu zaidi lakini pia lenye uhakika wa mabao mengi.

Hata hivyo, 'nafuu' hapa ina maana ya zaidi ya euro 70 milioni, kiwango ambacho kilikubaliwa kati ya uongozi wa Sporting na mchezaji, wakikumbuka kwamba kiangazi cha mwaka jana Gyokeres aliweka presha kubwa akitaka kwenda kujiunga na timu hiyo inayojiandaa kucheza nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya PSG. Mkataba wake Lisbon unamalizika mwaka 2028.

Chelsea wapo macho. Wanajua Gyokeres angependa kwenda Arsenal, Liverpool au Manchester City, lakini pia wanajua kwamba Stamford Bridge si chaguo linalokataliwa na mchezaji huyo wa Sweden, hivyo wako tayari kumpandia dau.

Iwapo Gyokeres ataondoka, Sporting watafanya kila liwezekanalo kumbakiza Hjulmand. Kocha Rui Borges alipohojiwa kama usajili wa Kochorashvili una uhusiano na mshawasha kwa kiungo huyo Mdenmark alisema: "Jambo moja halihusiani na jingine. Wachezaji wana vifungu vya kuachwa, hiyo ni zaidi ya uwezo wangu. Ni mchezaji tunayemuamini sana. Kuhusu ubora wa Hjulmand, anaweza kucheza kwenye ligi yoyote kutokana na ubora wake binafsi, uwezo wake wa uongozi, tabia na haiba yake. Kwa hiyo ni mchezaji mzuri sana, na ni jambo la kawaida kusikia tetesi kutoka klabu mbalimbali Ulaya nzima."


Ollie Watkins

LIVERPOOL inafuatilia kwa karibu hali ya mshambuliaji wa England, Ollie Watkins wa Aston Villa, huku ikipanga kumsajili kama mbadala wa mshambuliaji wa Newcastle na Sweden, Alexander Isak, 25. Watkins, 29, amepigwa benchi katika mechi nne kati ya tano za Villa za mwezi Aprili, huku Marcus Rashford sasa akionekana kuwa chaguo la kwanza mbele yake. Arsenal ilibaniwa na Villa Januari ilipojaribu kumnunua Watkins, na sasa Liverpool wanaweza kuingia kwenye ushindani huo katika dirisha la kiangazi. Watkins ana mkataba na Villa hadi Juni 2028, aliosaini miezi 18 iliyopita.


Rasmus Hojlund

MANCHESTER United imeweka bei ya takriban Euro 65 milioni kwa mshambuliaji wa Denmark, Rasmus Hojlund, 22, huku klabu kadhaa zikiwa na nia ya kumsajili katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Vyanzo vya karibu vinasema United iko tayari kumuacha aondoke iwapo klabu inayomhitaji italipa bei hiyo. Klabu za Juventus, Inter Milan na Napoli zinaonyesha nia ya kumnasa.


Kim Min-jae

CHELSEA na Newcastle zimewasiliana juu ya uwezekano wa kumpata beki wa kati wa Korea Kusini, Kim Min-jae, mwenye miaka 28, kutoka Bayern Munich. Miaka miwili baada ya kujiunga na Bayern kutoka Napoli kwa Euro 50 milioni, Kim ameonyesha nia ya kutafuta changamoto mpya. Ingawa bado ana mkataba hadi 2028, anapendelea kuhamia ligi mpya, huku Ligi Kuu England ikiwa chaguo lake kuu. Msimu huu amecheza mechi 42 na kufunga mabao 3.


Antoine Semenyo

MANCHESTER United iko mstari wa mbele kumsajili mshambuliaji wa Bournemouth na Ghana, Antoine Semenyo, 25, lakini inakabiliwa na ushindani kutoka Liverpool na Tottenham. Bournemouth hawako tayari kumwachia kwa urahisi na wanamtathmini kwa hadi Pauni 70 milioni. Semenyo, aliyefunga mabao 11 msimu huu, ana mkataba wa miaka minne zaidi.


Samuel Chukwueze

FULHAM bado inavutiwa na winga wa AC Milan na Nigeria, Samuel Chukwueze, mwenye miaka 25, baada ya kushindwa kumsajili Januari. Chukwueze alikaribia kujiunga na Fulham siku ya mwisho ya dirisha la usajili, lakini makubaliano hayakufikiwa. Safari yake AC Milan haijakuwa na mafanikio na klabu iko tayari kumuuza kwa kati ya Euro 12–15 milioni. Klabu za Hispania kama Real Sociedad na Real Betis zinavutiwa naye pia.


Tyler Dibling

MANCHESTER United itakomalia mpango wa kumsajili kiungo wa kati wa Southampton, Tyler Dibling, 19, iwapo itafuzu ushiriki wa Ligi ya Mabingwa Ulaya kupitia ubingwa wa Europa League. Southampton inataka ada ya usajili ya hadi Oauni 100 milioni. Dibling pia anavutiwa na klabu nyingine kama Chelsea, Manchester City, Tottenham, Bayern Munich, na RB Leipzig.


Morgan Gibbs-White

MANCHESTER City iko mbele katika harakati za kumsajili kiungo mshambuliaji wa Nottingham Forest, Morgan Gibbs-White, mwenye miaka 25. Februari mosi 2025, Gibbs alifunga bao katika mechi yake ya 100 kwa klabu hiyo kwenye ushindi wa 7–0 dhidi ya Brighton. Mkataba wake unaisha Juni 30, 2027.