Uncle Shamte ajitoa ishu ya Mzee Nyange

MUME wa mama mzazi wa msanii wa Bongofleva, Diamond Platnumz anayefahamika kwa jina la Uncle Shamte amesema mgogoro wa Mama Diamond na wanaotajwa kuwa baba wa mtoto wake haumuhusu.
Wiki iliyokwisha mama Diamond ambaye jina lake kamili ni Sanura Kassim alifichua kwamba baba mzazi wa msanii Diamond sio, Abdul Isack kama ambavyo wengi walikuwa wakifahamu, bali ni mzee anayefahamika kwa jina la Salum Nyange kwa sasa ni marehemu.
Baada ya mama kutoboa siri hiyo mitandao ya kijamii ilichafuka baada ya kila shabiki na mdau kujaribu kutoa maoni yake kuhusu habari nzima.
Akijibu swali la mwandishi lililouliza namna siri alifichua mama Dangote ilivyomgusa, Uncle Shamte amesema haijabadilisha chochote kwenye maisha yake kwa sababu ni kitu kilichotokea kabla hajajuana na mke wake.
“Miimi naona ni kama hakinuhusu, kinahusu mama na mtoto na baba. Yanayonihusu kuhusu mke wangu yanaanzia pale tuliopoanza uhusuanio wetu,” alisema Uncle Shamte.
Uncle Shamte na mama Diamond walifunga ndoa ya kimya kimya mwishoni mwa mwaka 2017 kwahiyo mpaka sasa wanatimiza miaka mitatu ya ndoa.