Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Afande Sele, 20 Parcent kumaliza bifu Valentine Day

AFANDE Pict

Muktasari:

  • Sasa bana, wasanii hao baada ya kutengana kwa kipindi chote hicho, Afande anafunguka chanzo na hadi kufikia kufanya shoo pamoja katika Siku ya Wapendanao, Februari 14, kwenye Ukumbi wa Ding Tozzy Apartments uliopo Nyashishi, jijini Mwanza.

UNAKUMBUKA lile bifu la Afade Sele na 20 Percent? Wasanii hao wa Bongo Fleva walikuwa hawasemeshani kwa zaidi ya miaka 10 kwa madai mkali huyo wa Hip Hop aliona kama mkali wa Afrobeats anataka kumpanda kichwani.

Sasa bana, wasanii hao baada ya kutengana kwa kipindi chote hicho, Afande anafunguka chanzo na hadi kufikia kufanya shoo pamoja katika Siku ya Wapendanao, Februari 14, kwenye Ukumbi wa Ding Tozzy Apartments uliopo Nyashishi, jijini Mwanza.

Akizungumza na safu hii ya Dakika 5 Na... Afande Sele ambaye ni msimamizi wa shoo hiyo anasema hakuwa na maelewano na 20 Percent kwa miaka 10, ishu kubwa ni mambo aliyokuwa anamwambia kama ushauri aliona ni kama anataka kumpanda kichwani, ingawa kwa sasa kila kitu kiko sawa na wana kazi ya pamoja wanaandaa.

"Unajua sikuwahi kuwa na bifu kubwa na 20 Percent, ila zilitokea tofauti ndogo ambazo mimi kama kaka yake nikaona nijitenge naye mbali. Sababu kuna mambo alikuwa akinieleza nilikuwa naona kama anataka kunipanda kichwani na ukikaa chini kufikiria ni ushauri mzuri tu alikuwa anaitoa kwangu," anasema Afande Sele na kuongeza;

AFA 02

"Kwanza alikuwa ananishauri niache kunywa pombe ama nipunguze, hii ilikuwa tangu nilipofiwa na mke wangu wa kwanza mama Tunda, sasa mimi nikawa kama naona ananizingua, alikuwa ananiambia pia suala la kuoa nikawa napingana naye sana, yaani ushauri wake haukuwa mbaya ila nikaona mikae naye tu mbali.

"Huweziamini 20 Percent ni mmoja ya watu wanaonimudu, sasa nilipooa nikaona tutaenda sawa na ndio nikamtafuta ili tukaweke sawa tofauti zetu Siku ya Wapendanao (Valentine Day), maana siku hii haimaanishi tu wale waliokuwa wapenzi bali hata wasio wapenzi lakini wanaishi kwa upendo basi inawahusu, hivyo tutapanda kuimba jukwaa moja nyimbo zote tulizoshirikiana naye," anasema Afande Sele ambaye kwa sasa yupo kwenye ndoa baada ya miaka 11.

Kuhusu shoo hiyo ya Siku ya Wapendanao, Afande Sele anasema imeandaliwa na mdau wa muziki Ding Tozzy kwa kuwakusanya nyota wa Bongo Fleva, Mr Blue, MB Dogy, 20 Percent na msanii anayechipukia katika miondoko ya Singeli, Mama Amina.

AFA 03

KAZI YA PAMOJA

Afande anasema pia mbali na shoo hiyo pia kuna mkakati wa kufanya kazi kwa pamoja na 20 Percent ambayo tayari wameshaianza kuiandaa.

"Na kuonyesha tupo pamoja, tumeamua kuwapa zawadi mashabiki zetu kwa kutoa kazi mpya ya pamoja mimi na 20 Percent, hivyo kuna kazi mpya inakuja ambayo tayari tumeshaanza kuiandaa, hivyo mashabiki wasubirie ujio wetu si unajua hatuna kazi mbovu sisi," anasema nyota  huyo anayeshikilia taji la Mkali wa Rhymes lililofanyika mara moja tu zaidi ya miaka 15 iliyopita.

AFA 04

Sababu ya kuwachagua wakali hao

"Mimi kama msimamizi  wa shoo, ukiachana na mratibu wetu Ding Tozzy, nimeamua kumchangua 20 Parcent sababu nimefanya nae baadhi ya nyimbo kwa pamoja na nyimbo anazoimba yeye zinafanana jumbe sawa, hivyo nimeona itapenda pale jukwaani tukipanda pamoja."

"Kwa MB Dog nimeangalia nyimbo zake nyingi ni za mapenzi na hii ni shoo ya wapenda nao, hivyo ni sehemu sahihi yeye kuwepo kwa siku hiyo pale  Ding Tozzy Apartments."

"Sasa kwa Mr Blue, nimeangalia ni mwanamuziki ambaye anafanya muziki wa kizazi chote, anafanya kizazi cha zamani na kizazi hiki cha sasa, yaani katika shoo hii atakuwa  anaunganisha mashabiki wa aina zote pale jukwaani."

"Kwa upande wa Mama Amina, kwanza nimeona kumpa sapoti kwa kile anachokifanta, yaani amethubutu na ameweza bila ya kujali changamoto yoyote aliyonayo kwenye kipaji chake na nataka jamii ithamini kipaji chake bila ya kujali tatizo la kuongea alilonalo."

AFA 05

Mr Blue, 20 Percent, MB Dogy wafunguka

“Valentine ni siku ya mapenzi na muziki wangu umekuwa ukizungumzia sana mapenzi na maisha. Hii shoo ni muhimu na fursa kwangu kuwapa burudani halisi ya Bongo Fleva mashabiki wangu waliokuwa nami tangu mwanzo,” anasema Mr Blue.

“Hii siyo shoo ya kawaida, ni kukumbusha watu tulikotoka na namna muziki ulivyokuwa na ujumbe, Valentine hii tunarudisha burudani halisi pale Ding Tozzy Apartments, Mwanza," anasema MB Dogy, huku 20 Percent akasema; “Mashabiki wetu wamekuwa wakituuliza lini tutapanda jukwaa tena. Valentine hii tunakuja na nyimbo zetu zote walizozipenda, ni shoo ya hisia na kumbukumbu.”

AFA 06

MRATIBU ATOA SABABU

Muandaaji wa shoo hiyo, Ding Tozzy anasema maandalizi yapo katika hatua za mwisho mwisho na tayari wasanii wote wanaendelea na mazoezi.

"Itakuwa ni zaidi ya shoo, kifupi wakazi wa Mwanza na wapenda burudani kali kote nchini wasipange kuikosa," anasema.