Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Barua zamiminika Diddy asamehewe

Muktasari:


  • Kesi ya P Diddy ilianza rasmi Septemba 16, 2024, alipokamatwa na kupelekwa mahakamani kwa mashtaka ya usafirishaji wa watu kwa ajili ya ukahaba na usafirishaji wa utumwa wa ngono.

MKONGWE wa muziki wa Hip Hop na mmiliki wa lebo ya Bad Boy Records, Sean Combs maarufu P Diddy ipo mikononi mwa mahakama ikisubiri hukumu itakayotolewa Oktoba 3 mwaka huu.

Kesi ya P Diddy ilianza rasmi Septemba 16, 2024, alipokamatwa na kupelekwa mahakamani kwa mashtaka ya usafirishaji wa watu kwa ajili ya ukahaba na usafirishaji wa utumwa wa ngono.

Baada ya kusomewa mashtaka, Diddy kupitia kwa mawakili wake walikana mashtaka yote, wakisisitiza kwamba mkongwe huyo alisingiziwa.

Miezi michache baadaye waendesha mashtaka waliwasilisha hoja kwamba Diddy ana nguvu kubwa kifedha na uhusiano wa kimataifa, hivyo anaweza kutoroka. Mahakama ikakataa kumpa dhamana ikiamua abaki gerezani akisubiri kesi.

Julai 2 mwaka huu, jopo la majaji lilimuondoa hatiani Diddy kwenye mashtaka makubwa mawili, lakini likamkuta na hatia ya usafirishaji kwa lengo la kushiriki ukahaba, ambalo ni kosa dogo zaidi kisheria.

Sasa kinachozungumzwa zaidi kwa sasa si kesi yake bali ni namna mastaa, familia na marafiki zake wa karibu wanaowasilisha barua mahakamni ili kupunguziwa hukumu hiyo inayotarajiwa kusomwa Oktoba 3.


MAPENDEKEZO YA KIFUNGO

Kuna mvutano mkubwa kati ya upande wa mashtaka na utetezi kuhusu muda wa kifungo, waendesha mashtaka wanapendekeza kifungo cha miezi 51–63 lakini upande wa utetezi unadai miongozo ya sheria inapendekeza miaka 2 tu.

Timu ya mawakili wa Diddy imeomba apewe kifungo cha miezi 14 pekee, hoja kwa sasa ni kwamba je, jaji ataangalia sheria au atafuata barua za watu wake wa karibu kama kigezo cha kupunguza ukali wa adhabu?


WALIOANDIKA BARUA

Miongoni mwa watu waliotuma barua ni mpenzi wa zamani wa Diddy na rapa wa Marekani, Caresha Romeka Brownlee maarufu Yung Miami, waliokuwa kwenye uhusiano tangu mwaka 2021 hadi 2024 alipokamatwa.

Yung Miami alisema mkongwe huyo alimfungulia milango kwenye kazi yake ya muziki na kujulikana akimtaja kuwa ni mtu mwenye upendo kwa watu:

"Alinifungulia milango na kunisaidia kukua, siwezi kuzungumzia yaliyotokea kabla sijamjua, lakini Diddy ninayemjua ni mtu mwenye upendo, mkweli na anayehamasisha, alinisaidia kukua binafsi na kitaaluma," anasema na kuongeza:

"Alitufungulia milango kwa wasanii weusi ambao awali tulikataliwa kwa miaka mingi, alinipeleka Met Gala kwa mara ya kwanza. Huu ni ushahidi wangu wa kujitolea kwake."

Mama mzazi wa Diddy, Janice Combs, mwenye miaka 84 anasema kabla hajafariki anatamani kuwa na mwanae kwenye kipindi cha mwisho ili awe karibu na familia yake:

"Nataka kutumia miaka yangu ya mwisho nikiwa na mwanangu, siwezi kusema nitakuwa hai kwa muda gani lakini natamani nimwone akiwa karibu na familia yake na watoto wake tena."

Inaelezwa hizo ni kati ya barua zilizogusa zaidi mioyo ya watu, mama huyo akieleza ugumu wanaopitia watoto wa Diddy kwa sasa.

Dallas Austin, mtayarishaji wa muziki, alimtetea Diddy na kusema ni mtu aliyefanya mabadiliko makubwa kwenye muziki hivyo kupunguziwa adhabu itakuwa msaada mkubwa kwake na kurudi kusaidia wasanii wachanga.

"Mtu wa mabadiliko kwenye muziki ni kama rafiki, naangalia ushawishi chanya aliokuwa nao. Amewasaidia wasanii wengi na mara kwa mara tulikuwa tukizungumza jinsi ya kuwa wanaume bora. Aliniuliza ninawezaje kuwa mtu bora na kuhusika zaidi kwenye jamii?"

Baadhi ya ngoma alizotengeneza Dallas ni pamoja na Don’t Take It Personal ya Monica, Damaged ya TLC, Don’t Let Me Get Me ya Pink, Secret ya Madonna na nyinginezo.

Stevie Jordan ‘Stevie J’, mtayarishaji wa zamani wa Bad Boy Records, anasema licha ya kupitia changamoto za dawa za kulevya kwa pamoja bado rapa huyo ana moyo wa kipekee:

"Diddy alibadilisha maisha yangu tangu tulipokutana studio miaka ya 1990. Licha ya mambo ya kazi, alinisaidia hata kifamilia akigharamia mazishi ya baba yangu. Hii ni ishara ya moyo wake."

Wengine waliomba kulegezewa kwa hukumu ya Diddy ni mzazi mwenzake, Sarah Chapman, alisema kifungo kimemfanya mkali huyo kuwa na akili tulivu mbali na misukosuko ya maisha ya starehe.

Dana Tran, mama wa mtoto wake mdogo Love mwenye miaka 2, alisema"Kutokuwepo kwake kumeathiri sana malezi. Huu ni wakati muhimu kwa mtoto wetu kumwona baba yake."

Quincy Brown, mtoto aliyemlea tangu akiwa mdogo, alisema: "Diddy ndiye baba pekee niliyewahi kumpata, sio mkamilifu, lakini ni mtu mwenye moyo wa upendo."

Sasa swali ni je, barua hizo zinaweza kubadilisha hukumu au adhabu kupunguzwa kutokana na watu mbalimbali kuandika ujumbe.

Kwa sasa, jiji la New York na dunia kwa ujumla inasubiri kuona uamuzi wa Jaji Arun Subramanian, je, ataangalia sheria inavyotaka na kumtia kifungo cha miaka minne au zaidi au atasikiliza sauti za familia na marafiki wanaoamini Diddy amebadilika?