Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Marseille, nyingine mbili zamnyatia kiungo Serengeti Boys

Muktasari:

  • Chole aling'ara katika kikosi cha Serengeti Boys kilichoweka historia kwa kufika hatua ya katika Fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya miaka 17 (AFCON U-17) na kukata tiketi y kufuzu Kombe la Dunia la U-17.

KIUNGO mahiri wa Serengeti Boys na mchezaji bora AFCON U-17, Issah Chole ameingia katika rada za miamba ya Ufaransa, Olympique de Marseille ikitajwa kuwa miongoni mwa klabu zinazomfuatilia kwa karibu.

Chole aling'ara katika kikosi cha Serengeti Boys kilichoweka historia kwa kufika hatua ya katika Fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya miaka 17 (AFCON U-17) na kukata tiketi y kufuzu Kombe la Dunia la U-17.

Kiungo huyo aliibuka mchezaji bora wa mashindano huku mshambuliaji Serengeti Boys, Athanas Adam akiwa mfungaji bora baada ya kufunga mabao matatu.

Taarifa kutoka Morocco ambako mashindano hayo yalifanyika zinaeleza kuwa Marseille imekuwa ikifuatilia maendeleo ya Chole tangu hatua za makundi.

Uwezo wake wa kutawala eneo la kiungo, kutengeneza nafasi na kucheza kwa utulivu licha ya umri wake mdogo, umevutia maskauti wa klabu hiyo maarufu ya  Ligue 1.

Mbali na Marseille, mabingwa wa Czech, SK Slavia Prague, nao wameonyesha nia ya kumchukua nyota huyo. Taarifa zinaeleza klabu hiyo tayari imewasilisha ofa inayokadiriwa kufikia Dola 190,000 ambazo ni zaidi ya Sh 500 milioni.

Akizungumzia kiwango cha kinda huyo, Kocha wa Yanga Soccer School, Mohammed Badru alisema hana shaka Chole anaweza kupata nafasi katika soka la kimataifa kutokana na alichokionyesha kwenye mashindano hayo.

"Ameonyesha kiwango kikubwa na naamini si Marseille pekee, tunaweza kuona ofa za timu nyingi kubwa zikimiminika kwa sababu katika mashindano makubwa kama hayo huwa kunakuwa na maskauti wengi wanaofuatilia vipaji," alisema Badru.

Hata hivyo, kocha huyo amewataka wachezaji wa Serengeti Boys kutoruhusu sifa na umaarufu wa sasa kuwavuruga, badala yake waendelee kuweka mkazo katika maendeleo ya taaluma zao za soka.

Alisema ni muhimu kwa vijana hao kupata mazingira bora ya kukuza vipaji vyao, hususani katika akademi na klabu zenye mifumo imara ya maendeleo ya wachezaji ili waweze kufikia viwango vya juu zaidi.

Badru aliongeza kuwa iwapo kizazi hicho kitaandaliwa vizuri, ndani ya miaka minne hadi mitano Tanzania inaweza kuwa na kundi la wachezaji watakaokuwa nguzo muhimu katika timu za taifa na hata kucheza katika ligi kubwa duniani.

Kwa sasa macho ya wadau wa soka nchini yataendelea kuelekezwa kwa Chole huku ikisubiriwa kuona kama Marseille, Slavia Prague au klabu nyingine zitachukua hatua rasmi za kumsajili nyota huyo anayechukuliwa kuwa mmoja wa vipaji vinavyochipukia kwa kasi katika soka la Tanzania.