Tishio la Ebola laivurugia Taifa Stars Morocco
Muktasari:
- Uamuzi wa kufuta mechi hizo umefanywa na serikali ya Morocco kutokana na tishio la ugonjwa wa Ebola.
Mechi mbili za kimataifa za kirafiki za timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ dhidi ya Rwanda na Uganda zilizopangwa kuchezwa Juni 5 na Juni 9 mwaka huu zimefutwa.
Uamuzi wa kufuta mechi hizo umefanywa na serikali ya Morocco kutokana na tishio la ugonjwa wa Ebola.
Taifa Stars ilipanga kucheza na Juni 5 na dhidi ya Uganda kabla ya kuikabili Rwanda, Juni 9, mechi zote zikipangwa kuchezwa jijini Marrakech, Morocco.
Licha ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) bado haijathibisha taarifa hiyo, lakini Shirikisho la soka la Uganda limetoa taarifa za kuhairishwa kwa mechi hizo zilizotakiwa kuchezwa Morocco sambamba na Shirikisho la Soka la Madagascar limetoa taarifa ya kuhairisha kwa michezo yao
“Shirikisho la Soka la Madagascar limepokea taarifa kutoka kwa Shirikisho la Soka la Kifalme la Morocco ikitangaza kufutwa kwa mechi zote zilizopangwa katika mfululizo wa matukio ya kalenda ya FIFA yaliyotakiwa kufanyika nchini humo”.
“Uamuzi huu unafuatia maagizo kutoka kwa mamlaka za mitaa za Morocco, ambazo zilionyesha kuwa hakuna mechi zinazoweza kuchezwa wakati wa Juni 2026 kwa sababu za kiafya na usalama”.
“Kwa hivyo, mechi ya kirafiki kati ya Madagaska na Uganda, iliyopangwa kufanyika Juni 8, 2026, huko Marrakech, imefutwa”.