Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

BONGO MUSICS FACTS: Kuna utofauti mkubwa kati ya Billnass na Nandy

Muktasari:

  • Akiwa ameshinda tuzo, Billnass ni rapa namba mbili nchini anayepata namba kubwa katika majukwaa ya kusikiliza muziki wa kidijitali baada ya Darassa kutokea Classic Music Group (CMG). Fahamu zaidi.

NI miaka 10 sasa jina la Billnass limekuwa likizunguka katika Bongofleva akitoa ngoma kali, huku silaha yake kubwa ikiwa ni uwezo wa kutengeneza ladha (melodic rap) ya kipekee ambayo imefanya hata kushirikishwa na wasanii wengi.

Akiwa ameshinda tuzo, Billnass ni rapa namba mbili nchini anayepata namba kubwa katika majukwaa ya kusikiliza muziki wa kidijitali baada ya Darassa kutokea Classic Music Group (CMG). Fahamu zaidi.


1. Jina la Billnass limetokana na jina lake la kuzaliwa, William Nicholaus, yaani William (Bill) na Nicholaus (Nass) ambalo ni la Baba yake, ni kama walichofanya watu maarufu duniani kama Bill Clinton na Bill Gates ambao majina yao ya mwanzo ni William.

2. Billnass alitoka rasmi kimuziki chini lebo ya Rada Entertainment baada ya kuachia wimbo wake, Raha (2014) uliotengenezwa na Mesen Selekta huku akiwashirikisha TID na Naziz, mwanachama wa kundi la Necessary Noize kutokea Kenya.

Huu ilikuwa ni wimbo mwingine kwa TID na Naziz kushirikiana baada ya ule uitwao Watasema Sana (2006) ambao ulifanya vizuri kwa wakati wake. 


3. Wimbo huo (Raha) ulifanya vizuri na kumuwezesha Billnass kuwania vipengele viwili katika Tuzo za Muziki Tanzania (TMA) 2015 kikiwamo kile cha Msanii Bora Chipukizi ambacho ushindi ulienda kwa Barakah The Prince.


4. Bilnass alianza kuwika kimuziki akiwa bado mwanafunzi wa Chuo cha Biashara (CBE) ambapo mwaka 2017 ndipo alihitimu na kupata shahada ya ugavi na manunuzi, na chuoni hapo chuo ndipo alikutana na mkewe Nandy kwa mara ya kwanza.

5. Baada kufanya kazi na Rada Entertainment, L.F.L.G (Live First Live Good) na Rooftop Entertainment, Billnass alifungua lebo yake, Mafioso Inc ambayo tangu mwaka 2021 imekuwa ikisimamia kazi zake.


6. Kwa kufungua huko lebo, Billnass aliungana na wasanii wengine wa Hip Hop Bongo waliofanya hivyo kama Joh Makini (Makini Label), Fid Q (Cheusi Dawa Entertainment), Moni Centrozone (Majengo Sokoni), Darassa (Classic Music Group (CMG)) n.k.


7. Wimbo wa Billnass, Puuh (2022) akimshirkisha Jay Melody ndio ulimuwezesha rapa huyo kushinda tuzo yake ya kwanza TMA, ni katika kipengele cha Msanii Bora wa Kiume wa Hip Hop 2022 akiwabwaga Kala Jeremiah, Country Boy, Fid Q na Joh Makini.


8. Na mwaka huo ndipo Billnass alikuwa msanii wa pili wa Hip Hop Bongo aliyetazamwa zaidi katika mtandao wa YouTube, video zake zilitazamwa zaidi ya mara 25.9, huku akiwa ametanguliwa na Darassa aliyetazamwa mara milioni 28.6.

9. Billnass ameshiriki kuandika wimbo wa Nandy, Dah! (2024), na kwa ujumla wawili hao ambao ni wanandoa wameshirikiana katika nyimbo tano ambazo ni Bugana (2019), Do Me (2020), Party (2021), Bye (2022) na Totorimi (2024).


10. Ikiwa ni miaka 10 tangu ametoka kimuziki, Billnass hajatoa Albamu, EP, LP wala Mixtape kwa mashabiki wake!, yeye ni kuachia wimbo mmoja mmoja tu ikiwa ni tofauti kabisa na mkewe Nandy aliyetoka na wimbo wake, Nagusagusa (2016).


Nandy ameshatoa EP tatu, Taste (2021), Wanibariki (2021) na Maturity (2022) pamoja na albamu moja, The African Princess (2018) huku akishinda tuzo nne za TMA ikiwa ni sawa na Phina, Young Lunya na Marioo aliyemwandikia wimbo wake, Wasikundanganye (2017).