Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mambo matatu yanasubiriwa kwa  Jux kimataifa

JUX Pict

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa Jux alisema Nigeria zimefanyika harusi tisa za kitamaduni ukiachana na hapa Dar es Salaam na kijumla amefanya shughuli 10 za kitamaduni zote zikifanyika Nigeria.

KAMA ulikuwa unajua harusi ya msanii wa Bongo Fleva na muigizaji Priscilla Ojo imeisha basi jua wawili hao mambo hayajaisha na sherehe itahitimishwa hapa Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Jux alisema Nigeria zimefanyika harusi tisa za kitamaduni ukiachana na hapa Dar es Salaam na kijumla amefanya shughuli 10 za kitamaduni zote zikifanyika Nigeria.

Hadi sasa, Jux na Priscy wameweka rekodi ya harusi ndefu zaidi kwenye historia ya showbiz na kwa mujibu wa mama mzazi wa mwanadada huyo anasema harusi ya Dar itakuwa funga mwaka.

“Sita zimemalizika, mbili zinakuja moja Lagos na moja Tanzania hiyo ndio funga mwaka,” aliandika Iyabo Ojo kwenye mtandao wa Instagram.

JU 05

Wikiendi hii Jux alifunga ndoa ya kitamaduni , kikristo na Party Nigeria na mpenzi wake, Priscilla ndoa iliyohudhuriwa na mastaa kibao wa Afrika kuanzia waigizaji na wanamuziki.

Karibu mitandao yote ya kijamii sio Instagram, Facebook wala Tiktok zilienea habari za harusi ya wawili hao na wengine wakaenda mbali zaidi na kusema ilisimamisha albamu ya Davido na macho na masikio yakawa kwenye ndoa hiyo.

Nyota kama Korede Bello, Mercy Aigbe, Destiny Etiko, Mr P na Toyin Abraham ni miongoni mwa wasanii waliohudhuria harusi ya wawili hao.

JU 02

Kwa upande wa Jux, mastaa kama Diamond Platnumz, Ommy Dimpoz, D Voice, Nandy, Billnas, Gnako Irene Paul na wengineo walihudhuria sherehe hiyo na kumsindikiza nyota huyo wa R&B.

Ikumbukwe wawili hao walifunga rasmi ndoa Februari 07 mwaka huu jijini Dar es Salaam ikihudhuriwa na watu wachache akiwemo Diamond, Zuchu, Ommy Dimpoz, S2kizzy na familia ya Priscilla.

Sasa kwa namna moja ama nyingine ndoa hiyo inaweza kumnufaisha msanii huyo kwenye mambo matatu ambayo Mwanaspoti limekuchambulia chini.

JU 01


KOLABO ZA KIMATAIFA

Ukiachana na umaarufu wa Jux kwa Afrika Mashariki lakini ndoa hiyo inaweza kumpa kolabo za wasanii kutoka Afrika Magharibi ambao wanafanya vizuri duniani.

Kitendo cha kuwaalika wasanii mbalimbali wa Nigeria kwenye harusi hiyo ni wazi sio tu kuishia kufurahi lakini kuna kubadilishana mawasiliano. Nyota huyo amefanya kolabo mbili tu na wasanii wa Nigeria Singah kwenye wimbo wa Fashion Killer, Phyno ‘God Design’ alioutoa hivi karibuni.

JU 04

MUZIKI WAKE

Kuoa mwanadada huyo kutamuongezea mashabiki wa nchi hiyo ambao pengine hapo kabla hawakumjua na kuanza kusikiliza kazi zake kutokana na umaarufu wa Priscilla pia mengine yanayotarajiwa kutokea ni uboreshaji wa kazi zake na mbinu mpya za kukuza ubunifu.

Hivi karibuni ametoa ngoma ya ‘God Design’ ambayo ni mahususi kwa ajili ya ndoa yake lakini katika wimbo huo kuna mabadiliko makubwa ya sauti tofauti na ilivyozoeleka.

Wimbo huo umechanganywa lugha tatu Kiswahili, Kiingereza na baadhi ya lugha za Nigeria maarufu kama Hausa na Bura.

Ladha ya mziki huo umebadilika kabisa kutoka R$B ambao ndio muziki anaoimba msanii huyo hadi Afro Beat ambao nin maarufu zaidi Afrika na Duniani.

JU 03

Tangu awe na mahusiano na Priscilla, Jux amepata sapoti kubwa kutoka Nigeria kuanzia kwa mkwe wake, Iyabo Ojo na marafiki wake wa karibu.

Wimbo wa Ololufemi alioimba Jux na Diamond uliotoka miezi saba iliyopita ambao hadi sasa umefikisha watazamaji Milioni 16 Youtube, umepromotiwa na Iyabo kwenye mitandao yake ya kijamii.


KUKUZA BIASHARA YAKE

Mbali na kazi yake ya sanaa lakini Jux anamiliki chapa ya mavazi kwa jina la Africa Boy akiuza baadhi ya nguo za kiume. Hilo pia litamuongezea soko la kimataifa na chapa yake kujulikana sio tu kwa Afrika Mashariki na Nigeria.