Mbosso hajaridhika, apania makubwa zaidi
Muktasari:
- Mbosso ambaye hivi karibuni ameachika wimbo unaoitwa 'Darasa la Saba' aliliambia Mwanaspoti wengi wamekuwa wakidhani tayari amefika kileleni kutokana jitijada zake anazofanya kuhusu sanaa yake, lakini kwa mtazamo wake anaona bado ana malengo mengi ambayo hajayatimiza.
MSANII wa Bongo Fleva, Mbosso amesema pamoja na mafanikio aliyoyafikia, hajaridhika na anajiona kama bado yuko mwanzo wa safari yake ya muziki, huku akisisitiza kila hatua aliyopiga imekuwa ni daraja la kumfikisha kwenye hatua nyingine kubwa zaidi.
Mbosso ambaye hivi karibuni ameachika wimbo unaoitwa 'Darasa la Saba' aliliambia Mwanaspoti wengi wamekuwa wakidhani tayari amefika kileleni kutokana jitijada zake anazofanya kuhusu sanaa yake, lakini kwa mtazamo wake anaona bado ana malengo mengi ambayo hajayatimiza.
“Ni kweli nimepata mafanikio kwenye kazi yangu hii ya muziki, lakini bado nina njaa sana ya kufanya makubwa zaidi, nataka kuona muziki wa Kiswahili unafika mbali zaidi ya hapa tulipofika sasa,” amesema Mbosso.
Aidha amesema mafanikio hayo yametokana na nidhamu, kujituma na kujifunza kila siku na hakuwahi kujiona bora kuliko wengine bali alijiona kama mwanafunzi anayeendelea kujifunza katika kila hatua ya maisha yake ya sanaa.
Mbali na hayo, Mbosso aliwataka wasanii chipukizi kutokata tamaa wanapokutana na changamoto, kwani hakuna safari ya mafanikio isiyo na maumivu na vikwazo.
“Kinachotakiwa ni uvumilivu, nidhamu na kumwamini Mungu, ukiacha hapo mambo mengine yanajipanga yenyewe,” amesema Mbosso.