Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mkojani kula sahani moja na chipukizi

MKOJANI Pict

Muktasari:

  • Mkojani ambaye mara nyingi kazi zake anafanya na Tinwhite kama Ndani ya Mwezi wa Ramadhan, Mjomba, Timu Mbovu, Binadamu Wawili Wawili, Cha 2000 na nyingine nyingi, alisema atahakikisha wanakula sahani moja na chipukizi hao ili kuwapa mashabiki upana wa kuchagua kazi wanazozipenda.

MSANII wa vichekesho nchini, Mkojani amesema kufanya vizuri kwa chipukizi katika tasnia hiyo kunamsaidia kuwa mbunifu wa kuandaa kazi zake.

Mkojani ambaye mara nyingi kazi zake anafanya na Tinwhite kama Ndani ya Mwezi wa Ramadhan, Mjomba, Timu Mbovu, Binadamu Wawili Wawili, Cha 2000 na nyingine nyingi, alisema atahakikisha wanakula sahani moja na chipukizi hao ili kuwapa mashabiki upana wa kuchagua kazi wanazozipenda.

“Mashabiki wangu wajiandae kwa kucheka maana sina kazi mbovu, ninatoa mafunzo na kuburudisha na mwaka huu utakuwa wa mafanikio makubwa zaidi,” alisema Mkojani na kuongeza;

“Napenda kuangalia vichekesho vya wasanii chipukizi, wanafanya vizuri sana, wana ubunifu kikubwa tunakutana sokoni walaji wa kazi zetu wao ndio watachagua waangalie kazi zipi maana kila mmoja ana kitu anachokipenda zaidi.”

Alisema siyo kazi ndogo kuwafanya mashabiki kucheka kwani changamoto za kimaisha ni nyingi ila kitendo cha kila anapoachia kazi zake watu wanafurahia, kinazidi kumpa nguvu ya kujituma kwa bidii.

“Kwanza ukikaa na mimi muda wote utacheka, kwani siamini katika makasiriko maisha yanahitaji furaha na uhai ni zawadi tosha kutoka kwa Mwenyenzi Mungu,” alisema Mkojani shabiki wa Simba kindakindaki.