Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rupia afunga bao la 10, aizamisha Azam FC

RUPIA Pict

Muktasari:

  • Mchezo huo ulikuwa ni wa kisasi kwa Singida baada ya mechi ya mzunguko wa kwanza uliopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam, kuchapwa mabao 2-1, November 28, mwaka jana, huku bao la kufuatia machozi likifungwa pia na Elvis Rupia.

Bao la dakika ya 75 la Mkenya Elvis Rupia, limetosha kuipa pointi tatu muhimu Singida Black Stars katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya matajiri wa Jiji la Dar es Salaam Azam FC, uliopigwa kwenye Uwanja wa CCM Liti mjini Singida.

Mchezo huo ulikuwa ni wa kisasi kwa Singida baada ya mechi ya mzunguko wa kwanza uliopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam, kuchapwa mabao 2-1, November 28, mwaka jana, huku bao la kufuatia machozi likifungwa pia na Elvis Rupia.

Rupia alipachika bao hilo dakika ya 62, baada ya Azam FC kutangulia kupata mabao yao kupitia kwa Feisal Salum 'Fei Toto' dakika ya 38, huku la pili likiwekwa kimiani na mshambuliaji wa kikosi hicho raia wa Colombia, Jhonier Blanco dakika ya 56.

Ushindi kwa Singida unaifanya timu hiyo kuzidi kukoleza vita ya nafasi ya nne za juu, kwani imefikisha pointi 50, katika michezo 25, baada ya kushinda 15, sare mitano na kupoteza pia mitano, nyuma ya Azam FC inayopo nafasi ya tatu na pointi 51.

Pia, Singida imeendeleza wimbi la ushindi kwani imefikisha michezo mitano mfululizo ya Ligi Kuu bila ya kupoteza, tangu mara ya mwisho ilipochapwa mabao 2-1, dhidi ya mabingwa watetezi Yanga, kwenye Uwanja wa KMC Complex Mwenge Februari 2, 2025.  

Kwa upande wa Azam FC, hiki ni kichapo cha nne msimu huu katika Ligi Kuu Bara, baada ya kushinda 15 na kutoka sare sita, huku ikikabiliwa na mchezo mgumu ujao wa 'Mzizima Derby', dhidi ya mabingwa watetezi Yanga, utakaopigwa Alhamisi hii ya Aprili 10.

Bao la Rupia la leo, linamfanya nyota huyo kufikisha mabao 10 ya Ligi Kuu Bara msimu huu, akizidiwa moja na Clement Mzize na Prince wa Yanga wenye 11, nyuma ya kinara, Jean Charles Ahoua wa Simba anayeongoza hadi sasa na mabao 12.

*****