Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sakata la Harmonize na Ibraah lafika pabaya

IBRAH Pict

Muktasari:

  • Maneno hayo yametoka nje ya madai ya Sh1 bilioni na kuhamia kwenye mambo yao binafsi na kusababisha taharuki mitandaoni kutokana majibizano ambayo yameanza kukolea leo Mei 11, 2025.

Sakata linalomuhusu msanii Ibraah kutaka kuchangiwa Sh1 bilioni na watu ili aondoke kwenye lebo ya Konde Gang inayomilikiwa na Harmonize limefika pabaya baada ya kuanza kutoleana maneno mabaya ya kujibizana kupitia mitandao.

Maneno hayo yametoka nje ya madai ya Sh1 bilioni na kuhamia kwenye mambo yao binafsi na kusababisha taharuki mitandaoni kutokana majibizano ambayo yameanza kukolea leo Mei 11, 2025.

Harmonize aliandika: "Nimemchunguza sana mdogo wangu Chinga nimegundua ana roho **** na kama sio ibilisi amempanda kichwani, maana hata siku aliyoposti na kusema namdai 1.B ni ile siku ya birthday ya mjukuu wangu Amarah, yaani mimi na kipenzi changu tunatrendi, kifupi alisikia wivu guys, sijamuomba Chinga bilioni ila mkataba alio-sign na lebo unasema ikitokea watu wanataka kumnunua wenye malengo makubwa zaidi ya Konde Gang. Pengine tunaweza tofautiana kipato, inatakiwa ailipe label ya Konde Gang 1.B ili wawasaidie vijana wengine na nilimwambia nitabaki kuwa kaka yako na Konde Gang chama lako, this guy have 2 pay, mchangieni, nililipa kwa kukopa."

Baada ya kuandika hivyo, muda huo huo Ibraah naye akamjibu Harmonize kwa kuscreen shot andiko hilo na kuliposti kwenye akaunti yake akiandika:

"Sitokusifu roho mbaya na wala sitokutangazia mabaya yako na ndio maana hata waandishi wa habari nawakwepa maana sitamani kuona unaandikwa vibaya kwenye mitandao ya kijamii. Wewe ni kioo ila chenye ukungu, lakini pia ninachoamini msaada wako katika maisha yangu ni mkubwa, umenisaidia sana kaka Konde, pia nikiendelea kujibizana na wewe mtu ambaye hata mama yangu aliyenizaa unataka ***** kikatili wakati nguvu za kumpambania ninazo Kaka Konde na bado unakaa kunitangazia ubaya, sema nini kakaangu asante maana hata nikiongea mimi masikini kauli yangu haifanani na ya kwako tajiri, na najua lengo lako ni nikose kabisa msaada ili nije tena kukuomba pango ***** bro MIMI NI MSELA. Naendelea kukutunzia maovu yako mengine sababu naamini utabaki kuwa kaka 🙏🏿🙏🏿"@harmonize_tz

Andiko hilo la Ibraah limezua taharuki mitandaoni kutokana na maneno aliyoyaandika huku watu wengi wakitaka watumie busara kwa kumalizana salama na sio kutoleana maneno yasiyofaa.