Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Zaiy Lissa kwa Manara ngoma ngumu, kwa makabila ilikuwa hivi

Muktasari:

  • Zaiy Lissa ambaye anatamba kwenye tamthilia ya Jua Kali, alipiga stori na Mwanaspoti katika Dakika 5 Na... na kufunguka yanayohusu ndoa yake na kile kinachoongelewa kwenye mitandao ya kijamii ambayo pia mwandishi alitaka kufahamu ukweli wake.

MOJA ya ndoa zinazotazamwa zaidi kwa sasa ni ya Haji Manara na Zaiy Lissa. Ikiwa ndiyo kwanza inatimiza mwaka mmoja mengiu yamezungumzwa hasa kwenye mitandao ya kijamii ingawa hayo yanayosemwa wenye majibu na ufafanuzi ni wawili hao.

Zaiy Lissa ambaye anatamba kwenye tamthilia ya Jua Kali, alipiga stori na Mwanaspoti katika Dakika 5 Na... na kufunguka yanayohusu ndoa yake na kile kinachoongelewa kwenye mitandao ya kijamii ambayo pia mwandishi alitaka kufahamu ukweli wake.

Anasema hadi wanamaliza mwaka sasa, ndoa yao iko imara na haijawahi kutetereka tofauti na wengi wanavyofikiria.


Ndani ya mwaka mmoja umejifunza nini katika ndoa?

“Aise, nimejifunza mambo mengi ya maisha baada ya kuingia kwenye ndoa. Yaani nachukulia ndoa yangu kama chuo cha mafunzo kwa jinsi nilivyobadilika na kuwa tofauti na nilivyokuwa nje ya ndoa hii. Nimekuwa tofauti kabisa. Sasa hivi kila kitu nakifanya kwa ustaarabu kwa kuwa najiona nimekuwa mwenye majukumu mengi, pia nimejua kuishi na watu wanafki wasionitakia mema.”

Haya ndiyo anayoyataka

“Mimi naomba Mungu atujaalie miaka mingi ya kuwa pamoja kama mke na mume InshaAllah. Ndoa yetu aijaze kıla kheri, baraka, masikilizano, upendo, furaha na maelewano na atujaalie riziki zilizokuwa za halali, ukweli nampenda sana mume wangu amenionyesha maana halisi ya mwanamume. Yaani Haji sio mume tu ni mume bora, kitu ambacho sijawahi kukiona kwa yeyote, Ukiacha kwa wazazi Wangu.


Wazushi... mmemsikia lakini...

“Kingine, nawaomba baadhi ya watu waache mara moja kuizungumzia ndoa yangu vibaya, kwani niwahakikishie tu hii ndoa ina cheti cha serikali, hakuna yeyote anayeweza kuivunja, labda sisi wenyewe, hivyo maneno ya uzushi uzushi kila wakati embu wayaache.”


Changamoto gani unapata kwenye ndoa?

“Sina changamoto yeyote mimi na mume wangu Haji. Tunaishi kwa amani kabisa ndani ya nyumba. Maisha yangu ya ndoa ni matamu kwa kweli, sijajutia kuingia kwenye ndoa, namshukuru Mungu kwa hilo. Ila kuna wale watu wanaofosi  ndoa yetu iwe na changamoto, wale vizabizabina vinavyojileta kutaka maneno ya hapa na pale, aise wasichanganye maisha yao ya mitandaoni na maisha ya ndoa yangu, wawe wapole tu.”

Vipi kuhusu kupata mtoto?

“Napenda sana watoto. Ni suala la majaaliwa ya Mungu kuzaa na Haji, japo nina mtoto mbali na Haji na Haji ana watoto pia na tunawalea bila kuonyesha utofauti.”


Zay Lissa ni mtu wa aina gani?

“Mimi ni mtu ninayependa sana kufurahi na kuwa na amani wakati wote. Pia ni mtu ninayependa hata watu wanaonizunguka wawe na furaha, ndiyo na mimi nafurahi, napenda kubembelezwa na nina hasira pia mtu akinikwaza.”


Katika tamthilia, msanii gani anakuvutia kufanya naye kazi?

“Kwa kweli mimi huwa nafurahi kufanya kazi na msanii yeyote nitakayepangwa naye kwenye kipande chochote cha kazi ‘Scene’.


Msanii gani unatamani ufikie levo yake?

“Mmh! Hakuna msanii anayeniumiza kichwa kwenye sanaa yetu, zaidi huwa naumiza kichwa changu mwenyewe, kwa sababu nataka nifike sehemu fulani.”


Neno moja kwenye ndoa yako

“Wenye roho za chuki, husda, choyo, wivu na uchawi wameshindwa kututenganisha na Haji hadi sasa, maana walitupa miezi mitatu sasa tumefikisha mwaka wasitarajie kama tutaachana, maana wamesubiri weeee, lakini wapi, Mungu yupo nasi wameumbuka.”

Vipi kuhusu kwenda kwa Dulla Makabila ?

“Sitaki hizi habari, maana zinashusha heshima ya ndoa yangu. Unajua kuna watu wako tu kukutia doa kwenye kitu fulani. Eti siku ya sherehe ya Hamisa na Azizi KI nilipotoka nilienda kwa Dulla, hivi nawezaje kufanya hivyo na hali ya kuwa nilikuwa na mume wangu?

“Mbali na mume wangu nilikuwa na mkwe wangu, na hata nisingekuwa nao, nisingeweza kufanya hicho kitendo, mimi nilishamalizana na Dulla kitambo na sasa kila mmoja ana maisha yake. Watu kumuingiza EX kwenye ndoa yangu ni kunikosea adabu mimi na mume wangu.”


Lakini wewe na Dulla Makabila mnaelewana kwa sasa?

“Mie sina tatizo na mtu, embu niache bana.”