Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chama alivyopishana na medali za CAF

Muktasari:

  • Ni medali ya tatu Chama anapishana nayo baada ya kuondoka timu ambayo baadaye inaenda kucheza fainali.

KITENDO cha Simba kutinga fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, kinazidi kuipeperusha Ligi ya Tanzania kimataifa lakini kwa kiungo mshambuliaji, Clatous Chama anaikosa medali hiyo baada ya msimu huu kujiunga na Yanga.

Ni medali ya tatu Chama anapishana nayo baada ya kuondoka timu ambayo baadaye inaenda kucheza fainali.

Hii imewahi kutokea pia kwa mastaa wakubwa duniani ambao wamepishana na makombe makubwa ikiwamo Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwamo, Zlatan Ibrahimovic aliyeondoka Barcelona  na kujiunga na AC Milan mwaka 2010, huku Barca ikatwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa 2011.

Philippe Coutinho alikuwa na kiwango bora akiwa na Liverpool na Januari 2018 akajiunga na Barcelona kwa dau kubwa, msimu uliofuata, Liverpool ikafika fainali.

Kwa Chama ambaye alitamba na Simba kwenye michuano mbalimbali iliyoshiriki ikiwamo kuisaidia robo fainali tano za Africa.

Alijiunga na Simba akitokea Power Dynamo ya nchini kwao, Zambia msimu wa 2018/19 na alikuwa mmoja wa nyota tegemeo wa kikosi cha kwanza kilichocheza robo fainali hizo.

Alikuwa na rekodi nzuri ikiwamo ya kuingia kwenye orodha ya wafungaji bora 10 wa muda wote wa mashindano ya Caf akiwa na mabao 23 na kukaa nafasi ya saba, huku anayeongoza ni staa wa zamani wa TP Mazembe ya DR Congo, Tresor Mputu aliyefunga 39.

Ndiye mchezaji pekee wa Ligi Kuu Bara anayeongoza kwa kufunga mabao mengi Ligi ya Mabingwa Afrika na kumpiku nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta mwenye 21.

Hizi ni baadhi ya timu ambazo Chama alicheza lakini hakubeba kombe la michuano mikubwa Afrika na badala yake alipishana nayo.


RS BERKANE

Baada ya kuonyesha kiwango bora akiwa na Simba, Agosti 16, mwaka 2021 Chama aliuzwa kwenda RS Berkane ya Morocco  ambako hakudumu muda mrefu kwa sababu ya kutokupata nafasi ya kucheza na Januari 14, mwaka 2022, alirejea Simba.

Baada ya anaondoka Morocco Mei 21, 2022 Berkane ikabeba ubingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika kwa kuifunga Orlando Pirates kwa penalti 5-4 baada ya sare ya 1-1.


SIMBA

Msimu uliopita Simba ilipitisha fagio kwa benchi la ufundi pamoja na kuwaondoa baadhi ya nyota kama, Saido Ntibazonkiza, Luis Miquisone na kusajili wachezaji wapya kutoka mataifa mbalimbali hususani Afrika Magharibi ikisajili Charles Ahoua, Chamou Karaboue na Augustine Okejepha.

Lakini kwa Chama ilikuwa tofauti kidogo kwani baadhi ya viongozi walitamani kuendelea naye wakati ambao mkataba wake umeisha lakini Yanga iliwahi na kumsaini mkataba wa mwaka mmoja.

Kila ilipokaribia tamati ya mkataba wa Chama na Simba, Wananchi walipambana kuhakikisha wanapata saini ya nyota huyo lakini mambo hayakwenda sawa akaendelea kusalia Msimbazi na hatimaye msimu huu wakafanikiwa.

Lakini wakati Chama anakimbilia jangwani kupambania nafasi ya kucheza robo fainali pengine hata nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, akapishana tena na medali ya CAF.

Wikiendi iliyopita Simba ilitinga fainali na kiufupi tayari ina medali ya Kombe la Shirikisho na Chama kapishana na zali hilo tena akiishia kulitazama chama lake la zamani kwenye runinga.


YANGA

Matamanio makubwa ya Chama msimu huu tangu alipojiunga na Yanga ilikuwa kuvaa medali ya Ligi ya Mabingwa ambayo hajawahi kufanya hivyo katika maisha yake ya soka.

“Ndoto yangu ni kuchukua ubingwa wa Afrika kuliko hata kuwa mfungaji bora na naamini hilo, haikuwa bahati wakati najiunga na Berkane, wakati huo walichukua ubingwa lakini kwenye mechi za makundi nilicheza na nilisaidia timu kwa hiyo tutapambana na kuchukua ubingwa,” alisema Chama alipohojiwa na Yanga TV.

Ikumbukwe Chama alikuwa akihusishwa kujiunga na Yanga kila inapofika mwishoni mwa msimu, wananchi hao walimhitaji hasa kwenye mashindano ya kimataifa ambayo Mzambia huyo alikuwa bora.

Msimu 2022/23 Yanga ilicheza fainali ya Kombe la Shirikisho na kuibuka mshindi wa pili dhidi ya USM Alger ya Algeria baada ya matokeo ya jumla ya sare ya 2-2, wakifungwa mabao 2-1 Uwanja wa Mkapa kisha kupata ushindi wa bao 1-0 Algeria na waarabu hao wakanyakua ndoo kwa faida ya bao la ugenini.

Msimu uliofuata Yanga ikaishia hatua ya robo fainali ikitolewa kwa mikwaju ya penati na Mamelodi Sundown ya Afrika Kusini baada ya sare ya bila kufungana kwenye mechi zote mbili.

Sasa baada ya kutua msimu huu imeishia robo fainali na kinachosubiriwa ni kama ataendelea kuwa nao msimu ujao ili kusaka mataji hasa ya kimataifa inngawa kuna tetesi huenda akaondoka mkataba wake ukiisha mwisho wa msimu.