Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

KIJIWE CHA SALIM: Soka kabla ya nyavu golini ngumi zilipigwa

KIJIWE Pict

Muktasari:

  • Nyavu ambazo siku hizi zipo katika miundo na ukubwa tofauti zinatumika kwa mambo mengi na kati ya hayo ni kinga ya kutafunwa na mbu wanaoambukiza ugonjwa wa malaria.

KWA miaka nenda miaka rudi nyavu katika nchi mbalimbali zimekuwa zikimsaidia sana binadamu katika maisha yake ya kila siku.

Hii ni pamoja na kutumika katika michezo mbalimbali ya ndani na nje.

Nyavu ambazo siku hizi zipo katika miundo na ukubwa tofauti zinatumika kwa mambo mengi na kati ya hayo ni kinga ya kutafunwa na mbu wanaoambukiza ugonjwa wa malaria.

Lakini yapo matumizi mengine na kati ya hayo ni kwa kutega samaki wakubwa na wadogo baharini, kwenye mito na mabwawa, wanyama, ndege na vipepeo.

Kwa mujibu wa kumbukumbu za historia, nyavu ziliaza kutumika zaidi ya miaka 10,000 iliyopita kwa kuwinda wanyama na ndege na kuwanasa samaki. Nyavu za kale zilitengenezwa kwa kutumia magome ya mti, mizizi, majani na hata kinyesi cha baadhi ya wanyama.

KJ 01

Kwa miaka mingi magoli ya mpira wa miguu na michezo mingine hayakuwa na nyavu, yaani yalikuwa wazi kama kirimba (fremu) ya mlango au dirisha na hii ilisababisha mara nyingi kuwapo kwa mizozo, hasa katika michezo iliyokuwa na uhasama au ushindani mkubwa.

Mara nyingine mchezo ulilazimika kuvunjika kabla ya muda uliopangiwa au hata wachezaji kuingiana maungoni ulipotokea ubishi kwamba mpira ulipita ndani au nje ya goli. Hapa inafaa kukumbuka kwamba hii teknolojia ya video ambayo inatoa jawabu sahihi katika michezo imekuja kuanzia karne ya 20.

Lakini hatimaye palipatikana ufumbuzi wa angalau kupunguza migogoro katika michezo. Hii ilitokana na mhandisi mmoja wa Kiingereza, John Alexander Brodie (1858-1934) ambaye alikuwa ni mpenzi wa kandanda na raga alikuwa anafanya kazi katika mji wa Liverpool alitengeneza wavu wa goli katika mwaka 1889.

KJ 02

Brodie alikuja na uamuzi wa kutengeneza nyavu za mpira baada ya mechi ambayo timu yake ya Everton ilifungwa bao ambalo aliamini lilikuwa la mpira uliotoka nje.

Wakati ule michezo minngi yenye ushindani ilikuwa na vurugu juu ya kulikubali bao ambalo mpira ulikuwa wa mwendo wa kasi na kuwa sio rahisi kujua ni bao au sio bao.

Nyavu za kwanza ziliwekwa katika magoli ya Uwanja wa Bramall Lane wa klabu ya Shefiel United na mchezo wa kwanza ambao magoli yake yalikuwa na nyavu ulifanyika Oktoba 8, 1887.

KJ 05

Mchezo huu ulikuwa kati ya klabu ya Preston North End na Hyde ambao ulimalizika kwa Preston kushinda 26-0. Bei ya nyavu kwa goli moja wakati ule ilkuwa shilingi nne.

Mhandisi Brodie alifungua kiwanda cha kutengenezea nyavu na kutoa nyavu za magoli 60 pamoja na milingoti yake kwa Uwanja wa Wembley na viwanja vingine.

Hatimaye Chama cha Kandanda cha England kikaidhinisha matumizi ya nyavu kwenye magoli mnamo mwaka 1891 na mchezo mkubwa wa kwanza ambapo magoli yalikuwa na nyavu ulikuwa kati ya Arsenal na Chelsea Desemba 27, 1934 kwenye Uwanja wa Wembley.

Ukubwa na mtindo wa kuzitengeneza hizo nyavu kwa mchezo wa kandanda umekuwa  ukibadilika mara kwa mara na siku hizi zipo staili na ukubwa tofauti kwa michezo ya kimataifa ya wanaume na wanawake, watoto na kwa magoli madogo yanayotumika kwa mazoezi.

KJ 03 (1)

Baadaye katika mwaka 1863, Chama cha Kandanda cha England kikatunga sheria ya magoli kuwa na upana wa futi 24 na urefu wa futi 8, kiwango ambacho kinatumika hadi sasa na kwa hivyo nyavu zikatengenzwa kwa ukubwa huo.

Matumizi yake yalipokewa bila ya pingamizi na hasa na waamuzi ambao mara nyingi walijikuta wanasukumiwa makonde pale wanapolikubali au kulikataa goli lenye utata.

Siku hizi zipo kila aina ya nyavu na zilizosukwa kwa mtindo tofauti na zipo ambazo bei yake huwa hadi Sh2 milionikwa nyavu za goli moja.

Siku hizi kampuni za nchi mbalimbali zimo katika ushindani mkubwa wa kutengeneza aina tofauti za nyavu ili kuvutia soko. Matokeo yake nyavu zipo za rangi nyeusi, nyeupe, bluu, nyekundu na mchanganyiko.

KJ 03

Baadhi ya klabu katika nchi mbalimbali siku hizi hutengenezwa nyavu za magoli yao zenye rangi za moja ya sare ya klabu zao.

Katika kandanda vipo visa na mikasa, kama ilivyo katika michezo mengine. Kati ya hivi visa ni pale walipotokea magolikipa baada ya kustaafu kuomba ling'olewe goli na nyavu zake kwenye uwanja wa klabu hio na kukabidhiwa kama kumbukumbu.

Wapo magolikipa waliostaafu ambao walikubaliwa ombi hili na wakayachukua magoli moja na nyavu zake na kuweka katika uwanja wa nyumba zao kama kumbukumbu za kuwa karibu na goli ambalo lilitumia muda mrefu wa maisha yake kulilinda ili nyavu zisitikiswe.

Beki wa zamani wa Barcelona na timu ya taifa ya Hispania, Gerard Pique, alikuwa na kawaida ya kukata nyavu na kuondoka nazo kila timu yake iliposhinda mechi na kutwaa ubingwa.

Sijui hali itakuwaje akitokea na hapa kwetu golikipa aliyestaafu akatoa ombi hilo.