Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

NYUMA YA PAZIA: Rematando? Kilomita bado chache Santiago Bernabeu

PAZIA Pict

Muktasari:

  • Rematando pia likazungumzwa zaidi katika mitaa ya Madrid. kwamba Real Madrid wangeweza kufanya kile ambacho kuna wakati wanakifanya. Kulipa kisasi na kuua mechi kiajabu baada ya kupoteza pambano la kwanza. 

REMATANDO. Neno la Kihispaniola linalomaanisha kumaliza kazi. Kuua kila kitu. Jude Bellingham alituambia kwamba ndio neno ambalo lilikuwa linazungumzwa zaidi katika vyumba vya kubadilishia nguo katika viwanja vya mazoezi vya Real Madrid. 

Rematando pia likazungumzwa zaidi katika mitaa ya Madrid. kwamba Real Madrid wangeweza kufanya kile ambacho kuna wakati wanakifanya. Kulipa kisasi na kuua mechi kiajabu baada ya kupoteza pambano la kwanza. 

Walikuwa wameteketezwa na faulo mbili za mguu wa kulia wa Declan Rice na kisha mguu wa kushoto wa Mikel Merino pale katika Uwanja wa Emirates. 3-0. Baadaye wakaanza kujiapiza kwa neno “Rematando”. Kwamba wangeenda kugeuza matokeo na kuua mechi Santiago Bernabeu.

PAZ 01

Wakafunika paa. Wakapiga kelele nyingi. Basi lao likasindikizwa na farasi. Muda wote huo Arsenal walikuwa wametua. Hawaongei kitu. kama ilivyokuwa katika mechi ya kwanza, wachezaji wa Arsenal walikuwa wamejiandaa kukimbia kilomita nyingi uwanjani kuliko wale wa Real Madrid. Real Madrid hii inanikumbusha ile ya Galacticoz.

Ile ya kina Ronaldo de Lima, Luis Figo, Roberto Carlos, Raul Gonzalez na David Beckham. Majina ni makubwa, lakini yalikuwa yanategemewa kufanya maajabu kwa kila mtu kuonyesha uwezo wake uwanjani.

Hakuwa na timu. Kuna tofauti kati ya kuwa na timu na kuwa na mastaa wakubwa. Kabla ya hizi mechi mbili nilitabiri kwamba Arsenal angemchapa Real Madrid katika mechi zote mbili.

Emirates na Santiago Bernabeu. Sio uchawi. Nawatazama Arsenal kila siku na nawatazama Real Madrid kila siku wanapocheza kule Hispania.

PAZ 02

Arsenal wameingia katika mpira wa kisasa. Real Madrid bado hawajaingia katika mpira wa kisasa. Siku hizi Pep Guardiola ametufundisha kwamba timu bora ni ile ambayo inakuwa bora wakati haina mpira.

Ndani ya dakika 180 za Emirates na Santiago Bernabeu, Arsenal walikuwa bora zaidi wakiwa hawana mpira. Walirudi katika lango lao kwa haraka na kubana kila nafasi. Kama sio William Saliba kufanya kosa la bahati mbaya, basi Madrid wangetoka kapa kwa dakika zote 180.

Lakini hapo hapo Arsenal walikuwa wepesi wakati wakiwa na mpira na walikuwa na mianya mingi ya kumfikia Thibaut Courtous. Haishangazi kuona kipa huyo alifikiwa mara nyingi pale Emirates kiasi kwamba alikuwa mchezaji bora wa mechi kwa upande wa Real Madrid.

Unazungumzia kuhusu Arsenal kufunga mabao ya faulo ya Rice, lakini ukweli ni kwamba Arsenal walitengeneza nafasi nyingi za kufunga Emirates. Na hii inatokana na ukweli kwamba wao wamewahi katika mpira wa kisasa kuliko Madrid.

PAZ 03

Madrid haikuziba njia kwa pamoja. Arsenal wangekuwa na wakati mgumu kama wangecheza na Atletico Madrid, lakini sio Real Madrid. Unadhani kina Vinicius Junior na Kylian Mbappe wana juhudi za kulinda lango kama wanavyofanya juhudi za kusaka lango la adui? Hapana.

Mpira wa kisasa unataka uwiano sawa kati ya kushambulia na kujilinda. Madrid hawana uwiano huo. Usishangae kuona wamepigwa tano tano na Barcelona. Usishangae kuona mechi nyingi wakicheza na kina Real Mallorca, Las Palmas, Getafe na wengineo bado huwa wanaruhusu mabao.

Wale wataalamu wa kamari watakuambia namna ambavyo Madrid huwa inawaangusha katika jambo hilo la kuruhusu mabao. Na sio kuruhusu mabao tu, bado matokeo yao hayatabiriki sana kama ya Barcelona.

PAZ 04

Unaweza kuwa na Vinicius, Mbappe na Jude, lakini mpira wa kisasa unahitaji kucheza kitimu zaidi kuliko kutegemea maajabu ya mchezaji mmoja mmoja. Madrid bado hawajatengeneza timu ya kutisha inayocheza kitimu. Ina wachezaji hodari ambao wanaweza kuamua matokeo mmojammoja.

Wamelitupa taji la Ulaya na nadhani wanaweza kulitupa pia taji la La Liga. Nasikia wanahusishwa na Xabi Alonso endapo kama Caro Ancelotti akitimuliwa. Watakuwa wamefanya jambo la maana. Alonso atawafanya kina Mbappe kukimbia kilomita nyingi zaidi uwanjani. Kilomita za kuja kusaidia wenzao katika ulinzi.

Ni kama alivyowafanya Bayer Leverkusen kiasi cha msimu uliopita kuwapa taji lao la kwanza la Ligi Kuu Ujerumani. Hawa kina Alonso ndio vizazi vipya vya soka la kisasa baada ya Pep kuingiza huu mpira wa kukimbia kilomita nyingi.

Vinginevyo Rematando zitaishia mdomoni tu pale Santiago Bernabeu kama tulivyoona Jumatano usiku. Sio Arsenal tu, kuna timu nyingi nazishikia dhamana kwamba zinaweza kwenda Santiago Bernabeu na kupata matokeo. Hata Liverpool wangeweza kwenda Santiago na kupata matokeo.

PAZ 06

Hata PSG wangeweza kwenda Santiago na kupata matokeo. Wana uwiano mzuri wa kujilinda na kushambulia. Wakati mwingine nadiriki kusema kwamba hata Nottingham Forest wangeweza kwenda zao Santiago na kupata matokeo.

Kwa sasa nahisi tutasikia uvumi mwingi wa Real Madrid kumtaka Rice au Saliba. Mwisho wa siku inaweza isiwe dawa kubwa kama hawatampata kocha ambaye atawaingiza katika mpira mpya. Don Caro ni kocha ninayemheshimu, lakini nahisi kama anaanza kupitwa na wakati kadri ninavyoitazama Madrid inavyocheza msimu huu.

Madrid wanahitaji kukimbia kilomita nyingi kama ambavyo klabu nyingi kubwa za Ulaya zimekuwa zikifanya kwa sasa. Kutegemea majina ya kina Mbappe ni kurudi katika zama za Galacticoz ambapo wengi tunakumbuka kuwa hazikuwa zama za mafanikio kwa Madrid.

Watazame PSG. Wameachana na mpango wa mastaa wakubwa kina Mbappe, Neymar na Lionel Messi, lakini sasa wamefika katika hatua ya nusu fainali wakiwa na mastaa wa kawaida ambao wapo tayari kukimbia kwa kilomita nyingi uwanjani. Hivi ndivyo mpira wa kisasa unavyohitaji.